Facebook

Monday, 8 September 2014

Yanga kupinga maamuzi ya TFF juu ya Okwi.

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema utapinga
maamuzi ya kamati ya Sheria na Hadhi ya
Wachezaji kuhusiana na maamuzi yake ya
kumtangaza mchezaji wake, Emmanuel Okwi
kuwa huru.
Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ya Yanga, Sam
Mapande amesema kuwa hawajaridhishwa na
maamuzi hayo ambayo yanakinzana na shitaka
zima la mchezaji huyo.
Mapande amesema kuwa kamati ya TFF imeamua
sakata la Okwi kinyume na malalamiko yao kwani
hakukuwa na lalamiko la mchezaji huyo wa
Uganda kuhusiana na malipo ya fedha zake za
usajili.
Alisema kuwa cha kushangaza, kamati hiyo ya
TFF iliamua kusikiliza kesi ambayo haikuwa
mbele yao na kutoa maamuzi ambayo hata wao
wameshangazwa nayo.
“Kwanza kesi yenyewe ilikuwa haijamalizika,
walituambia tuwasilishe vielelezo kuhusiana na
kitendo cha mchezaji huyo kufanya mazungumzo
na klabu ya Misri, lakini cha kushangaza
maamuzi yametolewa, hili limetushangaza sana,”
alisema Mapande.
Alisema kuwa mazingira yalikuwa yameandaliwa
kuibeba Simba na Okwi kwani hata malalamiko
yao kwa Simba hayakusikilizwa. “Malalamiko yetu
yalikuwa wazi kabisa, yapo kimaandishi,
hatukuwai kulalamikiwa, suala la fedha za usajili
la Okwi limetoka wapi, kama lilikuwepo, mbona
hatujajulishwa kimaandishi kama utaratibu
ulivyo,” alisema.
Alisema kuwa Kamati hiyo kumruhusu mmoja wa
wajumbe wa kamati hiyo Zacharia Hans Pope
ambaye pia ni mwenyekiti wakamati ya usajili ya
Simba kuwemo katika kikao hicho kinyume na
taratibu za Fifa kupitia kifungu namba 19
kinachoeleza mgongano wa kimaslahI

0 comments:

Post a Comment