Wakati nchi kama Tanzania inapambana kujenga viwanja vya ndege ili ndege kubwa kama za Fastjet ziweze
kutua sehemu kama Musoma, Kigoma na Arusha baada ya kuweza kufanya
safari zake kwenye mikoa ya Kilimanjaro, Mbeya, Dar na Mwanza, ifuatayo
ni list ya viwanja vya ndege duniani ambayo hutoka kila mwaka.
Kiwanja kilichoshika namba moja kwa kuwa busy kuliko vyote duniani ni
kiwanja cha Atlanta Georgia Marekani wanakotoka mastaa kama rapper T.I
ambacho kwa mwaka 2013 pekee kimehudumia abiria milioni 94.4, namba
mbili inashikwa na Beijing Capital International Airport ambacho
kilihudumia abiria milioni 83.7
Kiwanja namba 3 ni cha London Heathrow Airport kilichobakia kwenye
nafasi hiihii ya mwaka jana ambapo kimehudumia abiria milioni 72.4 huku
kiwanja cha Tokyo Japan (Haneda) kikishika namba 4, cha tano ni Chicago
O’Hare International Airport nchini Marekani na cha sita ni Los Angeles
International Airport hukohuko Marekani.
Kiwanja cha ndege Dubai kimeshika namba 7 kutoka namba 10 mwaka uliopita
ambapo kimehudumia abiria milioni 66.4 ambapo kiwanja cha ndege cha
Paris kimeshuka nafasi moja kutoka ya 7 mwaka uliopita na kushika ya
nane mwaka huu, ya tisa imeshikwa na kiwanja cha ndege cha Dallas/Fort
na namba 10 imeshikwa na kiwanja cha Jakarta Indonesia.
Hii ripoti imefanywa kwa kuhusisha viwanja vya ndege karibu 2000 ndani
ya nchi 160 duniani ambapo kwenye mistari ya ziada, kiwanja cha ndege
cha Hong Kong kimebaki kushika namba moja kwa kusafirisha sana mizigo
duniani ambapo mwaka jana kilisafirisha karibu tani milioni 4.2
0 comments:
Post a Comment