Habari ya kusikitisha kutoka Rungwe Mbeya
inahusu kijana kuawa kwa hisia za ushirikina,
ukiangalia sababu ya hisia hizi inasitikisha
sana.
MATUKIO ya kujichukulia sheria
mikononi bado yanazidi kuyakumba
baadhi ya maeneo mkoani Mbeya
ambapo katika tukio hili kijana
Gabriel Mwasyebule miaka 39 ameuawa
na wananchi wenye hasira kali
wakimtuhumu kwa imani za
kishirikina.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,
Ahmed Msangi, amethibitisha kutokea
kwa kifo hicho na kumtaja marehemu
aliyetambulika kwa jina la Gabriel
Mwandemwa (Mwasyebule) mkazi wa
kijiji cha Ikamambande (Lwangwa)
Wilaya ya Rungwe aliuawa na watu
wasiofahamika kwa kukatwa na vitu
vyenye ncha kali sehemu za kichwani
na kifuani.
Alisema tukio hilo lilitokea siku
ya jumapili majira ya saa tano
asubuhi huko katika Kijiji cha
Ikamambande, kata ya Lwangwa,
Tarafa ya Busokelo, Wilaya ya
Rungwe, mkoaniMbeya
Alisema taarifa za awali zinadaiwa
kuwa, uongozi wa kimila kijijini
hapo uliitisha kikao cha dharura
ukihusisha viongozi wa vitongoji na
vijiji jirani na ndipo waliamua
kumtafuta na kumlazimisha marehemu
kuhudhuria katika kikao hicho na
kisha kuanza kumpiga na kupelekea
kifo chake.
Marehemu alisema alikuwa akituhumiwa
kuwa ni mshirikina kijijini hapo
kwa kuwa anawaroga watoto na kuwa
anajipatia mazao mengi ya mavuno ya
viazi na kujipatia pesa
zilizowezesha ujenzi wa nyumba yake
aliyoweka marumaru na Gipsam pia
kumiliki pikipiki moja huku
akitarajia baada ya mavuno mazuri
ya mwaka huu kununua gari la
kutembelea.
0 comments:
Post a Comment