Facebook

Saturday, 6 September 2014

Who is Emmanuel Okwi.???


Katika nchi aliyozaliwa Sunday Manara
"Computer",
nchi aliyozaliwa Abdallah "King"
Kibadeni,nchi
aliyozaliwa Hamis Thobias "Gaga", nchi
aliyozaliwa
Method Mogella "Fundi" nchi aliyozaliwa
Edibily
Lunyamila, nchi aliyozaliwa Mbwana
Samatta , bado
leo hii kuna mtu anawapindua pindua kama
chapati??!!
Nchi aliyozaliwa Zamoyoni Mogella kipenzi
cha
wana-Msimbazi ambacho hakijapata kutokea,
alipothubutu kuiacha Simba SC alifungiwa
mlango wa
kurejea mazima!! Leo hii Okwi anafunguliwa
mlango
wa kurejea Msimbazi?
Nchi aliyozaliwa Julius Nyerere hadi leo hii
bado
inatoa viongozi wa soka mbumbumbu?
Edibily Lunyamila ni maarufu Uganda kuliko
Emmanuel Okwi iweje Okwi awe maarufu
Tanzania!!!
Emmanuel Okwi anaihitaji zaidi Simba kuliko
Simba
SC inavyomuhitaji Okwi, Okwi anaihitaji zaidi
Tanzania kuliko nchi nyingine yoyote ni hapa
pekee
ndipo ambapo anweza kufanya haya
anayoyafanya
huku watu wakiacha shughuli zao na kwenda
kumpokea pale Uwanja wa Ndege wa
Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere.
Watanzania tunaishi maisha ya kukariri
tunadhani siku
zote jana inafanana na leo na hatimaye leo
itafanana
na kesho, tutaendelea kuota ndoto kila
kukicha,
wenzetu wanafikiri sisi tunawaza, wenzetu
wanapumzika sisi tulala, wenzetu wana
tazama sisi
tunaona
Emannuel Okwi alikuwepo wakati Simba
ikichuana na
TP Mazembe pale National Stadium kwa kuwa
wenzetu wanatazama badala ya kuona, kwa
kuwa
wanafikiri badala ya kuwaza wakamchukua
Mbwana
Samatta wakatuachia Okwi, leo hii Mbwana
anawapa
makombe anawapa furaha, huku Okwi akiwa
ni yule
yule alichobadilika ni umri tu.
Nina imani hata kule Uganda kuna mji una
sifa kama
za Sumbawanga na ndiko anakotokea Okwi,
piga hela
baba wajinga ndio waliwao maisha yanataka nini tena zaidi.Tutakuja kufungua macho muda umeshakwenda. Tunaishi kwa kuangalia kilicho bora badala ya kutengeneza kilichobora.Naamini kina Okwi wako wengi sana mchangani,wengine kumzidi hata Okwi. Simba inashindwa nini kuwekeza kwa vijana kama Ramadhani Singano "Messi". Tutaendelea kuwa kichwa cha Mwenda wa Zimu hadi aliyetabiriwa atakaporudi. Ahsanteni

Imeandaliwa na..
                           Katemi Methsela

0 comments:

Post a Comment