Wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram
wameuzingira mji wa Maiduguri , mji rasmi
wa jimbo la Borno Kaskazini Mashariki ya
Nigeria.
Wazee wa vijiji wametahadharisha kuwa jeshi
linahitaji kuweka ulinzi thabiditi katika mji huo
ambao una zaidi ya watu milioni 2 ili kuzuia
mashambulizi kutoka pande zote za mji huo.
Kundi hilo limeteka sehemu kadhaa ambazo
ziko umbali wa kilomita 50 kutoka Maiduguri.
Kadhalika kundi hilo lilitangaza maeneo
iliyoyateka kama himaya zao.
Serikali haijatoa tamko lolote kuhusu taarifa
iliyotolewa na wapiganaji hao.
Kwingineko wakaazi wa miji iliyozungukwa na
Boko Haram Kaskazini Mashariki ya Nigeria,
wameelezea hatari kubwa inayowakabili wakati
wamejipata katikati mwa makabiliano kati ya
wanajeshi wa serikali na wanamgambo hao.
Baadhi waliokwama katika maeneo yenye
milima wamelazimika kula majani kama
chakula.
Kwa siku kadhaa sasa jeshi limekuwa likijaribu
kuwasamabaratisha wapiganaji wa Boko Haram
kutoka mji wa Michika - mji ambao ni wa hivi
karibuni kudhibitiwa na wanamgambo hao.
Katika mji wa Michika watu wamekwama kati
ya mabomu ya jeshi la wanahewa Nigeria na
wapiganaji wa jihadi wanaomfyatulia risasi mtu
yoyote anayosogea, na kwa mara nyengine hata
kuwakata shingo waathiriwa.
Mwanamke mmoja amesema kwamba
watoto wengi wamekwama nyumbani mwake
na hawajui wazazi wao waliko.
Miongoni mwa walioukimbia mji huo na
kwenda katika milima iliyo karibu, sasa
wameishia kula majani. Mwanamume mmoja
amesema watu 7 wamefariki mahali
alipojificha, na hawawezi kuzikwa.
Wakati huo huo kundi la viongozi
wanaoheshimiwa wanasema Boko Haram
wameulenga mji mkubwa Kaskazini mashariki
mwa Nigeria, Maiduguri.
Viongozi hao wa Borno wanasema miji na vijiji
vilivyouzunguka mji huo tayari vimedhibitiwa
na wanamgambo hao.Kundi hilo limeshutumu
namna serikali inavyokabiliana na hali.
0 comments:
Post a Comment