Elimu ya sekondari katika ngazi ya Kidato cha
Kwanza hadi cha Nne imekuwa ikiongozwa na
michepuo ya ama ya Sanaa, Sayansi, Ufundi na
Biashara. Halika dhalika, masomo ya sekondari
Kidato cha Tano na Sita yamekuwa ya
kifundishwa kwa kutumia Tahasusi mbalimbali
kulinga na mahitaji ya nchi ambazo kwa sasa ni
PCM, PCB, PGM, CBG,EGM,CBA,CBG,CBN kwa
Sayansi, na HGL, HGK, HKL, KLF, ECA, HGE kwa
Sanaa.
Mafanikio mbalimbali yamepatikana kwa
kutumia mfumo huu tangu ulipoanza hadi sasa.
Hata hivyo, kutokana na (a) nia ya nchi kupiga
hatua zaidi katika maeneo mbalimbali ya
maendeleo ya nchi kwa mujibu wa Dira ya Taifa
ya Maendeleo 2025, (b) mabadiliko ya mahitaji
ya ulimwengu wa ajira na kazi na (c) kuendelea
kukua kwa ugunduzi na ubunifu pamoja na
matumizi ya Sayansi na Teknolojia katika
maeneo mbalimbali, Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi imeona kuna umuhimu wa
kupitia upya Michepuo na Tahasusi zilizopo ili
ufundishaji uweze kwenda na wakati. Michepuo
na Tahasusi hizo mpya zinatarajiwa kuanza
kutumika katika mwaka wa masomo
2015/2016.
Ili kufanikisha maboresho hayo, Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi inakaribisha
wadau wote wa Elimu na Mafunzo kutoa
mapendekezo ya jinsi gani Michepuo na
Tahasusi za elimu ya sekondari ziundwe au
kuanzishwa katika madarasa ya kidato cha
Kwanza hadi Nne na Tano hadi Sita. Mwisho wa
kutuma mapendekezo ni tarehe 31/10/2014.
Wadau wote mnahamasishwa kutoa maoni yenu
kupitia njia mbalimbali ikiwemo vikao ama kwa
kuwasiliana moja kwa moja na wizara.
Majumuisho ya mapendekezo ya tawekwa
kwenye magazeti na tovuti kwa maoni na hatua
za mwisho katika kukamilisha maboresho haya.
Mapendekezo ya Michepuo naTahasusi mpya
yatumwe kwa anuani ifuatayo:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
7 Mtaa wa Magogoni,
11479 DAR ES SALAAM.
"Elimu Bora Inawezekana; Timiza Wajibu Wako"
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA
UFUNDI
0 comments:
Post a Comment