Facebook

Saturday, 23 May 2015

DAR ES SALAAM YAPANGIWA SIKU 12 ZA UANDIKISHAJI WAPIGA KURA.

Hatimaye Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) imeweka hadharani ratiba nzima ya uandikishaji wa wapigakura kwa kutumia teknolojia ya Biometric voters Registration(BVR) huku mkoa wa Dsm ukipangiwa siku 12 tofauti na mwezi mmoja uliotumika ktk mikoa mingine.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo wakazi wa DSM wataanza kujiandikisha kuanzia tar 4 julai hadi julai 16 mwaka huu.

M/kiti wa NEC,Jaji mstaafu Damian Lubuva aliiambia mwananchi kuwa DSM imewekewa siku chache kwa kuwa mashine zote za BVR zilizokuwa mikoani zitakuwa zimeisharudishwa kufanikisha  mpango huo kwa haraka.

Jaji Lubuva alisema "ikitokea watu wakabaki wengi ndani ya siku zilizopangwa,ratiba hii siyo msahafu,tutaongeza siku kuhakikisha wanaandikishwa wote waliofika vituoni,na hii ni kwa nchi nzima."

Alisema jumanne hii walipokea mashine za BVR 1580 na kufanya idadi ya vifaa hivyo kufikia 6450,na kwamba umebaki mkupuo mmoja tu utakaokamilika mei 30 ili kuingiza mashine 1,550 ili kutimiza idadi ya mashine 8,000.

Iringa walianza April 29 na watamaliza 29/5,Rukwa kesho hadi hadi june 23,katavi 18/4 hadi juni 17, mikoa ya kigoma,singida,kagera na singida ilianza juzi na itamaliza siku moja baada ya katavi.

Mikoa ya geita,Mwanza,shinyanga na Simiyu itaanza kuandikisha june 2 hadi julai 4, wakati mikoa ya Arusha,Kilimanjaro,Mara na Manyara itaanza juni 12 hadi Julai 12.

Source:-Mwananchi

0 comments:

Post a Comment