Huyu ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi mwaka wa pili anayefahamika kama
Amim Lusekelo 'Ambassador of people' ambaye hapo jana aliamua kuandamana peke yake akiwa ameshikilia bango kubwa kuanzia Chuo kikuu Ardhi hadi bodi ya mikopo kisha akaelekea ofisi za Wizara Elimu.....Huu hapa chini ni waraka wake.
22/05/2015
WARAKA KWA WANA VYUO VIKUU TANZANIA
Ndugu zangu napenda kwanza nitoe pole kwa wanafunzi wenzangu wa vyuo vikuu kwa kupitia kipindi hiki kigumu ambacho serikali imechelewesha pesa za kujikimu(BOOM) lakini pia niwape pole wanafunzi wa vyuo ambao waliamua kusimama na kusema ukweli polisi wakawapiga mabomu na kuwanyanyasa.Pamoja na maandano yanayoendelea vyuo vikuu mbalimbali ili kueleza kuwa uvumilivu wa kusubiri hizo pesa umefika kikomo bila kuzaa matunda zaidi ya Chuo kikuu Dar-es-salaam(UDSM)...Baada ya wao kuungana kwa pamoja na kushinikiza serikali kutoa pesa hizo na zikatolewa siku hiyohiyo walioamua kutoingia darasani na wakapatiwa pesa ndani ya masaa 12.
Hivyo basi jana tarehe 21/05/2015...Mimi mwanafunzi kutoka chuo kikuu Ardhi LUSEKELO AMIMU(Ambassador of the people) nasoma mwaka wa pili.....Niliamua kuchukua uamuzi wa kuwa na safari ambayo nilitembea kwa miguu Toka Chuo kikuu Ardhi kuelekea Bodi ya Mikopo mpaka Wizara ya Elimu, safari hii ililenga kwenda kujua nini kinaendelea kuhusu swala hili kuchelewa kwa pesa kwa kipindi kirefu na kutokuwepo kwa Taarifa ya Serikali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania ya kueleza ni kwa nini pesa hiyo inachelewa.
Ujumbe wa Bango niliotembea nao ulikuwa unasema hivi��
"BAJETI YA ELIMU YA JUU YA MWAKA (2014/2015),INALIWA NA NANI? MBONA PESA HAZIONEKANI MPAKA SASA PESA HATUJAPATA(BOOM)? NANI MKOMBOZI WA ELIMU TANZANIA?"
Niliyokutana nayo katika safari hiyo ambayo ilinichukua takribani masaa mawili na nusu��
Nilianzia chuo kwa kuwaambia wanafunzi wenzangu wachache ambao muda wa asubuhi walikuwa wapo break time ya muda mfupi baada ya vipindi vya kwanza vya asubuhi kuisha. Niliwambia kuwa kwa hali ilivo sasa sio nzuri lazima tushinikize serikali itafute pesa kokote zilipo ili waweze kutupatia pesa kutokana na kauli ya Naibu Waziri wa fedha Mh:Mwigulu Nchemba kuagiza mamlaka husika zitupe hizo pesa mapema bila kufuata taratibu za kifedga nazani alitambua kuwa kuna umuhimu wa sisi kupata hizo pesa kwa wakati.
Na nikasema mm naanza safari kufika kwenye hizo mamlaka kujua wameishia wapi kuhusu utekelezaji wa kauli ya Mh:Waziri wa fedha.��
BODI YA MIKOPO
Wao walisema wazi kwamba mpaka sasa hawajapokea pesa kutoka hazina kwa ajili ya malipo hayo.
Hata kama wangekuwa wameipata pesa hiyo sizani kama wanaweza kukaa nayo ata masaa maana wanapokea malalamiko mengi kutoka kwa Wanafunzi vyuo vikuu mbalimbali.
Nikaondoka na kuanza safari kuelekea Wizara ya Elimu
WIZARA YA ELIMU
Nilipokuwa njiani nilipita katikati ya barabara kuu kutoka maeneo ya Mwenge kuelekea Posta iliko wizara ya Elimu na IKULU.
Nilipokuwa njiani nilipata ushirikiano wa watanzania walikuwa na usafiri wa magari yao kwa kuepuka pembeni.
Lakini kama kawaida ya polisi wa kutuliza ghasia(FFU)...Nilikutana nao mara mbili kwanza ilikuwa ni Maeneo ya Moroco..waliuliza unaandamana nikawambia hapana napeleka ujumbe huu!..Mara ya pili nikakutana nao maeneo ya Salenda bridge, hao waliuliza wewe vipi sikutaka kuwajibu ila baada ya kuona wanaendelea kuuliza nikawambia neno moja tu SAFI!
Nilipofika Posta jirani na Mahakama ya Kisutu...Nikakutana wa waandishi wa habari wa Clouds TV,,,,,walinihoji kuwa mbona unaandamana peke yako nikawambie napeleka ujumbe haya sio maandamano, walitaka kujua mimi ni nani na naelekea wapi nikawajibu kwa kuwaeleza nimetokea Bodi ya Mikopo naelekea Wizara ya Elimu na kama wao watashindwa kutolea maelezo ya ujumbe huu...Safari itaendelea kuelekea IKULU, kumuuliza na maswali ya ujumbe huo.
Nilipofika katika lango kuu la wizara ya Elimu, nilikaa getini hapo kwa masaa mawili lakini nikiwa hapo niliona watendaji wa wizara ya Elimu wakitoka ndani ya Ofisi zao na kuja kujua ujumbe wangu unasema nini?....Na wakichukua picha mbalimbali kwa kutumia simu zao.
Baada ya masaa mawili niliamua kuingia ndani ya ofisi hizo ila nikilenga kuonana na Waziri wa Elimu,,,,Nilipofika ofisini kwake niliambiwa kasafiri yupo nje ya nchi, Nikaelekezwa kwenda kwa katibu mkuu nae niliambiwa ametoka......Baada ya hapo nikaambiwa niende kwa MKURUGENZI WA ELIMU YA JUU!
MKURUGENZI WA ELIMU YA JUU��
Aliniambia ninaharaka naenda kwenye kikao nakusikiliza nikamwambia kama unaharaka huwezi kunielewa nasema nini....Ikabidi achukue utulivu na kunisikiliza nilimueleza wazi hali hii inafanya wanafunzi wa vyuo vikuu kuwa na mgogoro na serikali na kusababisha madhara makubwa kwa Taifa.
Majibu!
Ni kweli kwamba pesa hatuna mpaka hapa tunaangalia pesa tupate wapi na sisi tunaelewa mnawakati mgumu ila hatulali mpaka hapa naenda kwenye kikao kuhusu swala hilo maana nae mkurugenzi wa bodi ya mikopo yupo hapa kwenye hichi kikao tukishauriana namna ya kupata pesa hizo.
Na akasema kuna vyuo vikuu 14, ambavyo wanaenda kulipa pesa hizo na Chuo changu Ardhi kikiwemo kwenye Ordha hiyo..Lakini mpaka sasa pesa hatuna.
MCHAKATO WAO WA KUIPATA HIYO PESA��
Mpaka hazina haina pesa, hivyo basi Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na Bodi ya mikopo, wizara ya fedha...Wanamuomba IKULU(Rais na katibu), waiagize BOT iwapatie pesa hizo ili waweze kutulipa.
Hivyo lazima tujiulize kumbe kulikuwa hakuna pesa za kutupa mpaka itokee migomo ndo pesa itolewe?
Wao wameomba kuwa IKULU iwapatie pesa sisi kama wanazuoni naomba tutumie namna yoyote ile takayokuwa bora zaidi kuishinikiza IKULI(Rais), aagize hizo pesa zitolewe mapema sana sizani kama kuna uhitaji wa kuchukua mjadala au zaidi ya siku Tano kwa sababu mgogoro huu utashusha sana imani ya serikali kwa wanafunzi wa Elimu ya juu.
Binafsi nikajiuliza yafuatayo na Naomba kila mwanazuoni atafakari.
Vyuo vikuu vingi mwishoni mwa mwezi ujao na na mwanzoni mwa mwezi wa saba tunaenda kwenye mafunzo kwa vitendo(FIELD)...Je? kama hakuna pesa ya Elimu kutoka hazina mpaka iombwe BOT itoe pesa kupitia IKULU...Sasa wakati ukifika wa kwenda field pesa zitapatikana?
Kwa upande wa wakilishi wa wanafunzi wa ELIMU YA JUU, yaani viongozi wa serikali za Wanafunzi wamechukua hatua gani mpaka sasa hasa mwenye kiti wa Shilikiaho la vyuo vikuu Tanzani(TAHILISO)....Atoe msimamo mmoja kwa niaba ya wanavyuo vikuu Tanzania katika kuelekeza nguvu ya kushinikiza IKULU itoe hizo pesa mapema sana kupitia BOT.
Na wakishindwa kufanya ivo basi tuchukue uamuzi wanavyuo vikuu sisi wenyewe bila hao wawakilishi wetu kwenda mbele kuishinikiza serikali itoe pesa hizo mapema sana.
Pia natoa shukurani kwa DJ FETTY, kupitia kipindi cha Exexcel kinachoendeshwa na Clouds FM, ambapo aliripoti kuhusu matembezi yangu niliyoyafanya hiyo jana na yeye kuripoti katika kipindi chake
Maoni yako kama mwanazuoni kufanikisha hili kwa kuishinikiza serikali.Tuma maoni yako kwa kusema upo chuo gani? ww ni nani ?
Mawasiliano:
Simu:0684-615128
Watsap:0684-615128
Instagram:Ambassador of the people
Telegram: AmimuLusekelo
Facebook: Amimu Lusekelo
Email: lusekeloamimu@gmail.com
Imeandaliwa Na: LUSEKELO AMIMU(Ambassador of the people)-CHUO KIKUU ARDHI
"BAJETI YA ELIMU MWAKA 2014/2015, Inaliwa na nani?"
NANI MKOMBOZI WA ELIMU TANZANIA?
0 comments:
Post a Comment