Katika muonekano mpya wa ligi kuu Nchini Uingereza mwaka 1992 kumekuwa na utoaji tuzo kwa kocha aliefanya vyema zaidi katika msimu wa ligi pamoja na mchezaji.
Sir Alex Ferguson ni kinara akiwa amechukua tuzo hizo mara 11 akifuatiwa na Arsene Wenger aliechukua mara 3 sawa na Jose Mourinho kocha bora msimu huu wa 2014-15.
Harry Redknapp akiwa ndie kocha wa kwanza wa Uingereza kuchukua tuzo hizo 2009-10 amechukua mara 1 sawa na Allan Pardew pamoja na Tony Pulis kutoka Wales.
Kwa maana hiyo tuzo nyingi zimechukuliwa na raia wa Scotland mara 13 na kwa mbali ni Ufaransa na Ureno mara 3 wenye ligi Uingereza mara 2 visiwa vya Wales mara 1.
Kwa upande wa wachezaji Eden Hazard ndie mchezaji bora wa msimu huu akiwa ni Mbelgiji wa pili kutwaa baada ya Vicent Kampany wa Man City msimu wa 2011-12.
Fahamu Thierry Henry, Cristiano Ronaldo na Nemanja Vidic wamechukua mara 2 ni zaidi ya wachezaji wote walio wahi kuchezea EPL.
Baada ya kuoneka ni dhohofu kwenye tuzo za makocha kwa upande wa wachezaji Uingereza ni vinara kwa kuwa na tuzo 5 wakifuatiwa na Ufaransa mara 3 huku Ureno,Serbia,Ubelgiji wakizitwaa mara mbilimbili.
Manchester United ni vinara pia tuzo hizi zikitua mara 8 wakifuata Arsenal mara 4 wakati Liverpool na Chelsea wakitwaa mara 2 na kuziacha Sunderland,Blackburn, Manchester City na Spurs wakitwaa mara moja.
Hongera Jose Mourinho hongera Eden Hazard ikiwa ni tuzo yake ya tatu msimu
0 comments:
Post a Comment