Haya sasa naona mapazia ya vikombe yanafungwa rasmi siku ya leo pale Uingereza ndani dimba la Wembley
FA ndilo kombe la kwanza kuanzishwa kwenye medani ya soka 1871 kombe ambalo hushirikisha timu za ligi kuu na zile za madaraja ya chini na moja ya sifa yake miaka ya hivi karibuni ni vilabu vya ligi kuu kufanya vibaya pindi wakikutana na timu zilizo madaraja ya chini.
Mpaka sasa vinara wa kuchukua FA mara nyingi ni Manchester pamoja na mabingwa watetezi Arsenal wakiwa wamechukua mara 11 kwa maana hiyo Mzee Wenger na vijana wake watahitaji kuandika historia ya kuwa timu iliyo chukua mara nyingi zaidi.
Ukiachilia mbali hilo pia inakuwa ni fainal ya 19 kwa Arsenal na kuwa timu iliyo ingia fainal mara nyingi zaidi katika historia (1927,1930,
1932,1936,1950,1952,1971,1972,1978,1979,1980,1993,1998,2001,2002,2003,2005,2014,2015
Arsène Wenger, kasha chukua kombe hili mara 5-1998, 2002, 2003, 2005 and 2014 hivyo akifanikiwa kulichukua leo atakuwa kafikia rekodi ya kocha wa zamani wa Aston Villa George Ramsay alie chukua mara sita ubingwa huu 1887,1895, 1897,1905,1913, na1920.
Mara ya mwisho timu hizi zilipo kutana ni 2012, Villa mpaka mapumziko walikuwa wanaongoza 2-0 ila kibao kikageuka kwa Vijana wa Wenger kushinda 3-2 katika michezo 34 kwenye mashindano yote Arsenal ni wababe kwa kushinda mechi 22 na kutoa sare 9 na kupoteza michezo 3 pekee
Tim Sherwood ujio wake Aston Villa umekuja kipindi muhimu kwa timu hiyo ambayo imesha cheza fainal 10 za kombe hilo na ikichukua mara 7 mara ya mwisho ni 1957 ni kitambo sana tangu enzi zile Nyerere akiwa kwenye harakati za uhuru.
KONA KALI::
Tim Sherwood ni mpenzi wa 4-3-2-1 ambapo Benteke ndie jicho la timu nyuma yake huenda akamuweka kinda anae kuja vyema Grealish akisaidiana na Charles N'Zogbia au Gabby Abgonlahor ingawa kwa aina ya mchezo wa Arsenal ambapo Aston Villa watatumia mashambulizi ya kustukiza ni vyema aka anza Scott Sinclair ambae ana spidi na mtu hatari kwenye zoni ya adui.
Ashley Westwood,Delp na Cleverley watasimama kwenye safu ya kiungo wamekuwa si wabaya ila tatizo kubwa la vijana hawa Villa ni safu ya ulinzi ambayo imekuwa ikifanya makosa ya kizembe achilia mbali kukatika-katika sana na hilo linaweza kuwaliza mbele ya kina Sanchez.
Beki wa kulia Leandro Bacuna amekuwa mzuri sana kupandisha mashambulizi na mara nyingi krosi zake huwa hatarishi hivyo kazi ipo kwa Sanchez ambae ni dhaifu kukaba.
Presha ya Aston Villa itakuwa silaha kali mbele ya Arsenal ingawa ulinzi mbovu wa timu hiyo itakuwa shibe kwa vijana wa Wenger
Ngoja tusubiri kimbembe pale kati Santi Cazorla dhidi ya Jack Grealish.
Huku watazuia Benteke upande huu watakaba Giroud mwisho wa siku kuna Sanchez na Walcott , mpambanaji Delph na Sinclair.
KWA MAONI:
Choikangta ckt@gmail.com
0 comments:
Post a Comment