Facebook

Sunday, 31 May 2015

UCHAMBUZI FAINALI LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA Barcelona vs JUVENTUS Na Mr.CHOI.

   Naona siku zinazidi enda kufika kona kali na kama ilivyo hada tuliangazia upande wa baadhi ya historia muhimu zilizo wekwa na vilabu, wachezaji pamoja na makocha.

  MALDIN-Michuano ya Uefa inashika nafasi ya pili kwa kuwa na mvuto zaidi kwa mashabiki wa soka kwenye ngazi zote nyuma ya kombe la Dunia na upande wa ngazi ya vilabu inashika nafasi ya kwanza.

     CHOI- Ukiachilia mbali ubora wake kutoka na ushiriki wa timu bora pia moja ya sifa yake Mwamuzi anaechezesha michuano hii anatakiwa asizidi umri wa miaka 45 ili kuendana na kasi ya mchezo na taratibu hii ilipitishwa 1990.

    MALDIN- Ukiachilia mbali swala la umri pia mechi huchezeshwa na marefa watano achilia mbali wa mezani marefa wawili wameongezeka ambao husimama pembeni ya goli kwa lengo la kuangazia magoli tata na matukio mengine maeneo ya goli na hili lilikuja ama Uefa walipitisha na kutupilia mbali ( Goal Technology) kifaa maalumu cha kuangazi goli kinacho tumika kwenye baadhi ya ligi na mashindano ya Fifa.

CHOI- Kwanzia mwaka 1992 Uefa iliweka wastani wa kuwa na walau wadhamini nane kwenye michuano hii ambapo matangazo ya biashara huonekana kwenye mabango ndani ya uwanja na sehemu ya kufanyia mahojiano na kwa namna nyingine kwenye nyanja ya kujitangaza na kupata wadhamini wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa tofauti na huku kwetu tungali tumekosa ushawishi yakinifu na moja tatizo ni kutokuwa na timu  shindani nyingi.

   MALDIN- Ase yapo mengi na tukibaki eneo hilo la kibiashara kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya makampuni kutokuwekwa matangazo yao kwenye baadhi ya Nchi hasahasa makampuni ya vinywaji vikali na yale ya ubashiri kulingana na sheria za Nchi husika.
         Heinken ni moja ya kampuni ambayo matangazo yake hayawekwi kule Uturuki na kama unakumbuka  9 April 2013,Real Madrid hawakuvaa jezi yenye nembo ya mdhamini wao Bwin kwenye mechi dhidi ya Galatasaray-inIstanbul.

    CHOI- Nadhani safari halisia , msuli tuta ukaza kwanzia tarehe 1 kwa kuangazia wana fainali historia zao kwenye michuano hii bila kusahau engo za kila mchezaji.
     Usisahau kutizama mapato wanayo pata timu hizi mpaka bingwa hapo chini

.*KUFUDHU RAUNDI YA KWANZA:  €200,000

*.KUFUDHU RAUNDI YA PILI:
           €300,000

*.KUFUDHU RAUNDI YA TATU:
            €400,000

*.HATUA YA MTOANO:
             €3,000,000

*.MSHINDI HATUA YA MTOANO:  €2,000,000

*.HATUA YA MAKUNDI:
            €12,000,000

*.SARE HATUA YA MAKUNDI:
               €500,000

*.MSHINDI HATUA YA MAKUNDI:  €1,500,000

*.HATUA YA 16:
              €5,500,000

*.ROBO FAINAL:
              €6,000,000

*.NUSU FAINAL:
              €7,000,000

*.MSHINDI WA PILI:
              €10,500,000

*.BINGWA:
          €15,000,000

KWA MAONI::
Choikangta.ckt@gmail.com

0 comments:

Post a Comment