Rais wa Burundia Pierre Nkurunziza amehairisha uchaguzi wa ubunge
kwa siku kumi .
Msemaji wa rais Willy Nyamitwe ameiambia shirika la habari la AFP
kuwa kufuatia jaribio la mapinduzi juma lililopita na vurugu
zilizofuatia ni bora kuahirisha uchaguzi huo kwa muda.
''Uchaguzi huo wa ubunge ulikuwa umeratibiwa kufanyika tarehe 26
mwezi Mei lakini sasa inatubidi kuihairisha ili kuwasikiza washirika
wetu wa kimataifa pamoja na tume ya uchaguzi ambayo pia inatumia
muda huo kutatua maswali yaliyoulizwa na vyama vya upinzani.''
alisema Nyamitwe.
Hadi kufikia sasa tarehe rasmi ya uchaguzi wa urais uliopangwa
kufanywa Juni tarehe 26 haijabadilika.
''Subiri tu'' Nyamitwe aliwaambia waandishi wa habari.
Wanajeshi waaminifu kwa Nkurunziza walizima jaribio la mapinduzi
juma lililopita
Tayari rais Nkurunziza ametia sahihi amri hiyo ya kuhairishwa kwa uchaguzi.
Umoja wa mataifa ya bara Ulaya EU, na Umoja wa mataifa ya
Afrika AU, yametoa wito kwa uchaguzi huo uliokumbwa na utata
mkubwa uhairishwe ilikutoa fursa kwa mazungumzo ya upatanishi
kuendelea .
Hapo jana Rais wa Afrika Kusini alitilia pondo hoja hiyo ya kuahirisha
uchaguzi akisema ni bora uchaguzi huo uliopangwa ''uhairishwe''.
Takriban watu 20 wameuawa kufuatia makabiliano baina ya polisi na
waandamani katika mji mkuu wa Bujumbura kilele ikiwa ni juma
lililopita makamanda waasi walipotangaza jaribio la mapinduzi rais
Nkurunziza akiwa mjini Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa
viongozi wa kanda uliolenga kutatua mzozo wa kisiasa nchini mwake.
Waandamanaji wamekuwa wakipinga kauli ya Nkurunziza ya kutaka
kuwania muhula wa tatu
Wapinzani wa rais Nkurunziza wanasema kuwa kutangazwa kwake nia
ya kuwania muhula wa tatu unakiuka sheria na makubaliano ya amani
ya mwaka wa 2006 yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe
vilivyodumu kwa miaka 13.
Nkurunzizakwa upande wake anashikilia kukutu kuwa ana haki ya
kuwania muhula mwengine kwani muhula wa kwanza hakuchaguliwa na
wanainchi bali wabunge.
Takriban watu laki moja wamekimbilia mataifa jirani wakihofia
kutibuka upya kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
0 comments:
Post a Comment