Kundi la Boko haram limefanya mashambulizi katika mji wa Bama na kusababisha mauaji ya watu wengi huku wengine wakitoroka.
Wanamgambo hao waliuteka mji wa Bama ,ambao ni
wa pili kwa ukubwa katika jimbo la Borno siku ya Jumatatu baada ya
jaribio la awali la kutaka kuuteka mji huo kuzimwa na vikosi vya
serikali.Mamlaka ya Nigeria bado haijatoa tamko lolote kuhusu shambulizi hilo.
Taarifa zinasema kuwa watu wengi wametoroka wakiwemo wanajeshi.
Boko Haram walifika mapema asubuhi katika mji huo kwa magari ya kivita.Taarifa kutoka katika mji huo zinaeleza kwamba mashambulizi yalianzishwa na vikosi vya jeshi la Nigeria.
Msemaji wa kundi hilo la Boko Haram ameelezea hali ya mji huo kwa sasa kuwa wakaazi wa mji wa Bama wamekimbilia katika mji mwingine wa Borno na Maiduguri .
Nalo shirika la Amnesty International limetoa takwimu kuwa raia wapatao milioni nne wamekufa mwaka huu katika mgogoro huo kati ya Boko Haram na vikosi vya ulinzi vya Nigeria.
0 comments:
Post a Comment