Facebook

Tuesday, 2 September 2014

JUSTIN BEIBER ASHITAKIWA KWA UENDESHAJI MBAYA WA GARI


Ni jumanne nyingine,huku skendo nyingine ya Justin Beiber ikigonga vichwa vya watu mbalimbali.

Polisi wa Canada wanasema Justin ameshitakiwa kwa kuendesha gari vibaya pia kutoa lugha chafu.
Hii inafuatia baada ya gari lake kugongana na gari dogi {minivan} na kusababisha ugomvi huko Southwestern Ontario.

Yote hayo yalitokea siku ya Ijumaa mchana karibu na nyumbani kwa akina Justin ,Stratford lakini aliachiwa na kutakiwa kureport mahakamani tarehe Sept 29.

Hii si mara ya kwanza kwa Justin Beiber ,kwani alishawahi kushitakiwa kutokana na uendeshaji mbaya wa gari na kukataa kukamatwa baada ya kukimbizana na polisi huko Miami.

Ikiwa hiyo haitoshi alishitakiwa pia kwa kumkashifu dereva.Ingawa wanasheria wake walisema hana makosa yoyote.

Wapenzi wa Justin Beiber sasa hivi mioyo yao itakuwa ikienda mbio kwa sababu ya album aliyofanya na  Cody Simpson.

Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kupata taarifa mbalimbali zinazowahusu mastaa.

Imeandaliwa na....
                              SamChris Swai.

0 comments:

Post a Comment