Mario Balotelli ndio kwanza amerejea
England, kwa mara ya pili, lakini inaonekana
haijamchukua muda mrefu kugonga vichwa
vya habari, safari hii kwa kuonesha "ladha"
ya mitindo na mambo anayopenda.
Mchezaji huyo wa Liverpool aliyenunuliwa
kutoka AC Milan kwa pauni milioni 16,
amekuwa akitafuta nyumba, na inasemekana
ameichagua hii (katika picha) iliyopo nje ya
mji, - eneo la Helsby, Cheshire - na kufanya
ndio "keja".
Na kama picha hizi pamoja na habari ambazo
zimeandikwa na magazeti na tovuti kadhaa
hapa Uingereza ni za kuaminika, basi
inaonekana Balotelli ameonesha 'staili' yake
kwa 'kuteua' jumba hili ambalo thamani yake
ni pauni milioni 4.7.
Nyumba hii ina vyumba vitano, ikiwa pamoja
na kila kitu ambacho mchezaji soka , Kijana,
milionea anahitaji. Vitu 'muhimu' kama
bwawa la kuogelea, sauna, chumba cha
kuhifadhia mvinvyo (wine cellar), sehemu ya
kutua helikopta, uwanja wa mpira.. Na
vingine 'vidogovidogo'.
0 comments:
Post a Comment