Polisi nchini India wanasema
kuwa msichana mmoja ambaye alijaribu kumtetea babake kwenye baraza moja
la kijiji amepatikana akiwa amekufa.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 15 na babake
waliitwa na wazee wa kijiji katika eneo la Bengal Magharibi kutatua
mzozo kuhusu tingatinga.Palisi wanasema kuwa huenda msichana huyo alibakwa kabla ya kuuawa kwani mwili wake ulipatikana ukiwa uchi. Inaarifiwa msichana huyo alikejeliwa na wanakijiji kwenye baraza hilo kwa kuteta ambavyo babake alidhulumiwa.
Familia ya msichana huyo inasema kuwa alilazimishwa kutema mate ardhini na kuyaramba mate hayo, kitendo kinachoonekana kuwa cha unyama sana.
Mahakama zisizo rasmi nchini India hutoa adhabu dhidi ya wanakijiji wanaoonekana kuvunja sheria za kijiji kile.
Vitendo vya dhuluma dhidi ya wanawake nchini India vimeanza kumulikwa tangu ubakaji wa mwanafunzi mmoja mwaka 2012 kwenye basi la abiria.
Serikali ilidhibiti sheria za ubakaji mwaka jana baada ya maandamano makubwa kufuatia shambulizi hilo lakini unyanyapa dhidi ya wanawake bado ni janamizi.
0 comments:
Post a Comment