Mtangazaji
wa TV Piers Morgan ameacha kazi katika shirika la habari la Marekani la
CNN, licha ya kupewa nafasi ya kuongeza mkataba wake.
Morgan ame
tweet akisema anakwenda "kujaribu mambo mengine mapya" baada ya wakuu wa
kituo hicho kumtaka asalie kwa miaka miwili zaidi. Mkataba mpya ungempa
nafasi ya kuwa na mahojiano maalum ya vipindi 40.
Piers Morgan alimrithi Larry King, katika kipindi cha mahojiano, lakini kipindi hicho kilifutwa mwezi Machi kufuatia kupoteza umaarufu.
Kipindi kilianzishwa Januari 2011 kikiwa na watazamaji karibu milioni moja, lakini idadi hiyo ilipungua hadi kufikia 270,000.
"Nimekuwa na wakati mzuri katika kipindi cha miaka minne nikiwa na CNN,
na nina mheshimu sana Jeff [Zuckerberg, mkuu wa CNN] pamoja na watu
wote wanaofanya kazi hapo." Amesema Morgan.
0 comments:
Post a Comment