Watafiti wa afya kutoka Marekani
wameonya matumizi ya sigara za kielektroniki zilizoandaliwa kuwasaidia
wavutaji sigara kuacha uvutaji kwamba zinaweza kuwatumbukiza katika
matumizi ya dawa za kulevya.
Wanasema kuwa sigara hizo aina e-cigarettes ni
kweli zinaweza kupunguza madhara ya uunguaji wa tumbaku lakini zinaweza
kuleta madhara makubwa kama yale ya nicotine inayopatikana katika
tumbaku.Watalaam hawa wanasema mabadiliko ya mchangaiko huo unaweza kuleta madhara katika ubongo na pia unaweza kuwa chanzo cha hamasa kwa mtu kuvutiwa matumizi dawa za kulevya kama vile coccaine.
Ripoti ya utafiti iliyochapishwa katika jarida la the Journal of Medicine inasema madhara yanaweza kuwa makubwa zaidi kwa makundi ya vijana.
0 comments:
Post a Comment