Facebook

Tuesday, 2 September 2014

"Akili ya Wenger inavyokwenda tofauti na akili ya mashabiki."


Hivi ndivyo maamuzi, akili, moyo na msimamo wa mzee Wenger unavyokwenda kinyume na matarajio ya mashabiki wengi.
Baada ya tetesi nyingi kuhusu usajili huku Radamel Falcao na Edison Cavan wakiwa kwenye orodha yake,hatimaye
Arsenal wememchukua Danny Welbeck kwa kitita cha Paundi miloni 16 kutoka Manchester United.

Wenger amemchukua Welbeck ambaye hakuna hata shabiki mmoja aliyekuwa na imani kama siku moja ataweza kuchezea the Gunners.

Kwanini Wenger amewaacha kina Falcao,Cavana na kumchukua Welbeck hili ndo swali?
Mi nafikiri Wenger amemchukua Welbeck kwa sababu ni kijana na ana uzoefu na ligi kuu ya Uingereza.

Pili,Ni mchezaji mwenye nguvu na mwenye Uwezo wa 'kuhold' mipira na kusumbua mabeki wa timu pinzani mtu ambaye Arsenal
wamemkosa kwa muda mrefu tangu kuondoka kwa Fredy Ljumberg.

Uwezo huo utawapa mwanya viungo kina Ozil, Carzola na Ramsey kufunga.Vile vile swala la mshahara kwa watu kama kina Falcao ndiyo kikwazo kikubwa cha kutonunuliwa, kama utafanya uchunguzi Arsenal ni timu ambayo huwa inaendeshwa kwa bajeti ya hali ya juu ukilinganisha na timu kubwa za Uingereza.

Sishangai kusajiliwa kwa Welbeck bali nashangaa kwa nini Wenger hajasajili kiungo na beki au anadhani hapa Wenger sijui kwa nini
amepaacha hivo, au anamwandaa Coquelin bado kuna mashaka makubwa.
 

Nikikumbuka dhahama la msimu uliopita hasa kutokuwa na nguzo imara katikati,kiungo mkabaji tatizo ambalo hata Manchester United wanalo ila wamejaribu kumchukua Daley Blind.
Wenger atebaki kua mtu sahihi kwa Arsenal hata kama humtaki.Cha kufanya ni kuamini kile Afanyacho.Sina cha ziada, Karibu sana Emirates,
Welbeck japo hawakuamini lakini kuna kitu kipya utaleta.Wenger ni miongoni mwa waalimu wa soka wenye jicho la ziada katika kumuangalia mchezaji.

Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kupata uchambuzi wa matukio mbalimbali katika soka kupitia BantuTz SPORTS.
Imeandaliwa na......
                            Katemi Methsela.

0 comments:

Post a Comment