Facebook

Tuesday, 19 May 2015

Mourinho "Soka la Ulaya litabadilika endapo Messi atahama Barcelona"

Mpira wa bara la Ulaya utakuwa na mabadiliko makubwa sana kama
ikitokea Lionel Messi anaondoka Barcelona, hii ni kauli ya kocha wa
Chelsea Jose Mourinho.
Messi amekuwa ni mtu muhimu sana katika klabu ya Barcelona kwa
takribani muongo mmoja sasa, akiwasaidia kutwaa makombe matatu
ya ligi ya mabingwa Ulaya, makombe saba ya La Liga na mengine
kadhaa ambayo hayajatajwa.
Mourinho, ambaye alimpoka taji la La Liga Guardiola mwaka 2012
wakati akiinoa Real Madrid anahisi kuwa Muargentina huyo mwenye
umri wa miaka 27 ndio nguzo kubwa ya mafanikio ya klabu hiyo
"Ndani ya kipindi cha miaka 10 ambacho Messi hatokuwepo, ramani
ya soka la Ulaya lazima itabadilika sana," Mourinho aliiambia
talkSPORT.
"Walichoshinda Barcelona katika miaka kadhaa iliyopita wakiwa ama
na Frank Rijkaard, Pep Guardiola au Luis Enrique kama makocha ni
kwa sababu wamekuwa na kiumbe huyu."
Chelsea wamewahi kuhusishwa na kumwania Messi, ambaye kwa
wakati fulani alionekana kutokuwa na furaha klabuni hapo, lakini
Mourinho alikanusha vikali taarifa hizo.
Pia Jose Mourinho amesisitiza kuwa Barcelona na Real Madrid
zingekutana na kibarua kigumu kushinda kombe la ligi kuu England.
Soka la Hispania halimridhishi Mourinho akidai halina ushindani licha
ya yeye kushinda kombe la La Liga kwa rekodi ya pointi mia moja na
magoli 121 mwaka 2012 akiwa kocha wa Real Madrid.
Chelsea wametawazwa mabingwa wa ligi kuu zikisalia mechi tatu,
lakini Mourinho anadai wamefikia mafanikio kwa kutoa jasho
kwasababu England hakuna vitu rahisi kama La Liga.
Mourinho amesisitiza kuwa alipokuwa Hispania hakuwa na furaha
kwasababu alitwaa ubingwa kwa rekodi ya pointi na magoli mengi,
lakini alicheza mechi nne au tatu kwa msimu mzima.
Pia alipoteza ubingwa kwa pointi 92 huku akicheza tena mechi nne au
tano kwa msimu mzima.

0 comments:

Post a Comment