Ndege mbili za kijeshi
zinazobeba miili 40 kati ya 282 ya abiria wale waliofariki kutokana na
mkasa wa ndege ya Malaysia iliyodunguliwa huko mashariki mwa Ukraine ,
imewasili Uholanzi.
Theluthi mbili ya waliofariki kwenye mkasa huo
yaani 193 ni raia wa Uholanzi na nchi hiyo iko katika siku ya
maombolezi ya kitaifa na bendereza ziko nusu mlingoti.Bado haijaeleweka ni miili mingapi kati ya ile wa watu 282 waliouawa , imefikishwa hapo jana.
Maafisa wa kijasusi wa Marekani wamesema waasi wanaoiunga mkono Urusi waliitungua ndege hiyo kimakosa, lakini hakuna viashiria vyovyote kuhusu tukio hilo,vinavyohusiana moja kwa moja na Urusi.
Waasi wameshutumiwa kuwakwamisha wapelelezi kwa kuwapa ushahidi wenye mashaka na kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu idadi ya miili iliyopatikana.
Katika hatua nyingine maafisa wa nchini Malaysia wamekabidhi kisanduku cheusi chenye kurekodi mawasiliano ndani ya ndege kwa mamlaka za uholanzi.
0 comments:
Post a Comment