Mwanariadha raia wa Uingereza
mwenye asili ya Somalia, Mo Farah amejiondoa kutoka mashindano ya
Jumuiya ya Madola mjini Glasgow, Scotland.
Bingwa huyo mara mbili wa Olympiki amejiondoa
katika mashindano hayo ya jumuiya ya madola kutokana na ushindwa kupona
jeraha lake.“nimechukua uamuzi huu mgumu wa kujiondoa katika mashindano haya ya commonwealth “amesema mwanariadha huyo wa kikosi cha Uingereza.
“Ningependelea kuongeza medali ya commonwealth kwenye medali zangu za ubingwa wa olympiki na ubingwa wa dunia ,lakini mashindano haya yamekuja mapema wakati bado naenndelea kuuguza jeraha na mwili wangu bado haujanikubalia kukimbia”
Pia wachezaji wa Table Tennis kutoka Uganda na Kenya wanatupa karata zao katika michuano ya mchujo inayofanyika katika viwanja mbali mbali jijini Glasgow.
Kwingineko, kuna ripoti kuwa wanariadha katika kambi ya kikosi cha Kenya wanasemekana kulalamikia hali duni ya kambi yao.
Baadhi yao wanasema kuwa hawana vifaa vya kimsingi na hali katika kambi hiyo ni mbaya.
Vile vile wamelalamika kuhusu kucheleweshwa kwa marupurupu yao lakini maafisa katika kambi hiyo ya Kenya wamesema masuala hayo ni ya ndani na wanayashughulikia.
0 comments:
Post a Comment