Mamlaka nchini Sierra Leone
inataka usaidizi kutoka kwa raia wake ili kumsaka mgonjwa mmoja wa Ebola
ambaye alichukuliwa kwa lazima na familia yake katika hospitali moja ya
mji mkuu wa Freer Town.
Ni kisa cha kwanza cha ugonjwa huo katika mji
huo uliojaa idadi kubwa ya watu, na kwamba radio za taifa hilo zimetoa
habari zikiwaonya raia dhidi ya tishio la kumbukizwa iwapo watashikana
na mwanamke huyo.Kuna hofu kwamba ugonjwa wa Ebola huenda ukasambaa na kuingia nchini Nigeria.
Uchunguzi umethibitisha kwamba raia mmoja wa Liberia aliyefariki baada ya kutengwa katika hospitali moja ya Lagos alikuwa ameambukizwa ugonjwa huo.
Tangu kuzuka kwa ugonjwa huo mapema mwaka huu,zaidi raia 600 wamefariki kutokana na ugonjwa huo katika eneo la Afrika Magharibi.
0 comments:
Post a Comment