Thursday, 24 July 2014
Daktari wa Ebola apata maambukizi Sierra Leone.
Daktari anayeongoza vita dhidi ya ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone ameambukizwa virusi hivyo na sasa anatibiwa, imesema taarifa kutoka ikulu.
Vipimo kwa Sheik Umar Khan vilionesha ana virusi hivyo na amelazwa katika hospitali ya Kailahun, kwenye kitovu cha mlipuko wa ugonjwa huo.
Zaidi ya watu 630 wamekufa kutokana na Ebola katika mataifa matatu ya Afrika magharibi, tangu ulipojitokeza nchini Guinea mwezi Februari mwaka huu, zimeonesha takwimu za Umoja wa Mataifa.
Ni mlipuko hatari zaidi duniani wa ugonjwa na ambao hauna tiba
0 comments:
Post a Comment