RZ Pellets WAC 1-1 Chelsea
Wakati Chelsea inatoka Sare 1-1 kwenye Mechi ya Kirafiki na RZ Pellets huko Austria hapo Jana, Meneja wao José Mourinho amesema yupo tayari kumhuzunisha mmoja wa Makipa wao.
Petr Cech Jana alicheza baada ya kuwa nje kwa muda mrefu alipoumia Msimu uliopita
Lakini Chelsea wanakaribia kumkaribisha Kipa Thibaut Courtois aliekuwa huko Atletico Madrid kwa Mkopo kwa Misimu Mitatu.
Cech aliumia Mwezi Aprili kwenye Mechi ya UEFA
Chelsea
Ratiba/Matokeo Mechi za Kujipima Kabla Msimu mpya:
16 Julai Wycombe Wanderers 0-5 Chelsea
(Magoli: Bamford, Brown 2, Terry, Ivanovic)
19 Julai AFC Wimbledon 2-3 Chelsea , Kingsmeadow
23 Julai RZ Pellets WAC 1-1 Chelsea , Klagenfurt, Austria
27 Julai NK Olimpika Ljubljana v Chelsea, Ljubljana, Slovenia
30 Julai Vitesse Arnhem v Chelsea, Arnhem Stadium, Netherlands
3 Agosti Werder Bremen v Chelsea, Wesser Stadium, Germany
10 Agosti Ferencvaros v Chelsea, Albert Florian Stadium, Budapest, Hungary
12 Agosti Chelsea v Real Sociedad
Sporting Kansas City 1 Man City 4
Manchester City wameinyuka Sporting Kansas City Bao 4-1 kwenye Mechi ya Kirafiki iliyochezwa huko Kansas, USA Alfajiri hii.
Bao za City zilifungwa na Bruno Zuculini Dakika ya 3, Dedryck Boyata, 45, Kolarov, 72 na Iheanacho, 88.
Bao pekee la Kansas City C.J Sapong kwenye Dakika ya 30.
Hadi Mapumziko Bao zilikuwa 1-1.
Man City
Ratiba/Matokeo Mechi za Kujipima Kabla Msimu mpya:
13 Julai Dundee 2-0 Man City
18 Julai Heart of Midlothian 1-2 Man City (Sinclair, Kolarov)
23 Julai Sporting Kansas 1-4 Man City , Kansas, USA
Guinness International Champions Cup
27 Julai AC Milan v Man City, Heinz Field, USA
30 Julai Liverpool v Man City, New York, USA
2 Agosti Olympiacos v Man City, Bank Stadium, USA
Ngao ya Jamii
10 Agosti Man City v Arsenal, 17.00, Wembley Stadium
LIVERPOOL 0 AS ROMA 1
Bao la kujifunga mwenyewe la Daniel Agger limewapa ushindi AS Roma wa Bao 1-0 kwenye Mechi ya Kirafiki iliyochezwa huko Fenway Park Alfajiri hii.
Kila Meneja, Brendan Rodgers wa Liverpool na Rudi Garcia wa AS Roma, alishusha Kikosi kikali.
Lakini ni AS Roma ndio waliibuka kidedea kwa Bao la Dakika ya 90.
VIKOSI:
Liverpool: Jones, Kelly, Skrtel, Coates, Enrique, Lucas, Allen, Coutinho, Borini, Lambert, Ibe
AS Roma: Skorupski, Somma, Benatia, Castan, Cole, Florenzi, Keita, Nainggolan, Iturbe, Totti, Ljajic.
Ratiba/Matokeo Mechi za Kujipima Kabla Msimu mpya:
16 Julai Brondby 2-1 Liverpool (Peterson)
19 Julai Preston North End 1-2 Liverpool , Deepdale
23 Julai AS Roma 1-0 Liverpool , Boston, USA
Guinness International Champions Cup
27 Julai Olympiacos v Liverpool, Chicago, USA
30 Julai Manchester City v Liverpool, New York, USA
2 Agosti AC Milan v Liverpool, Charlotte, USA
10 Agosti: Liverpool v Borussia Dortmund, Anfield
LA Galaxy 0-7 Manchester United
WAKICHEZA Mechi ya Kirafiki, lakini ya kugombea Chevrolet Cup, Asubuhi hii Manchester United wameifunga LA Galaxy magoli 7-0 kwenye Uwanjani wa Rose Bowl, Pasadena, California mbele ya Mashabiki 86,432 katika Mechi ya kwanza chini ya Meneja wao mpya Louis van Gaal.
Nyota wa mchezo huo alikuwa ni Mchezaji mpya wa Man United Ander Herrera alietanda katikati ya Uwanja na kutoa pasi murua.
Bao za Man United zilifungwa na Danny Welbeck, Dakika ya 13, Rooney (Penati) 41’, na jingine 45’, Reece James, 62’ & 84’ na Ashley Young, 88’ & 90’.
Mechi inayofuata kwa Man United ni hapo Jumamosi Julai 26 dhidi ya AS Roma Sports Authority Field, Denver ikiwa ni Mechi ya Kundi A kugombea International Champions Cup.
VIKOSI:
LA GALAXY: Penedo; Gargan, Meyer, Leonardo, DLG; Ishizaki, Sarvas, Juninho, Husidic, Keane, Zardes
MANCHESTER UNITED: De Gea, Smalling, Jones, Evans, Valencia, Fletcher (c), Herrera, Shaw, Mata, Welbeck, Rooney.
[Zote Nchini Marekani]
**Saa za Bongo
Alhamisi 24 Julai 2014, Rose Bowl, Pasadena
Manchester United 7-0 LA Galaxy
Chevrolet FC Cup
Jumamosi 26 Julai 2014, Sports Authority Field, Denver
2306 Manchester United v AS Roma
International Champions Cup
Jumatano 30 Julai 2014, FedEx Field, Washington DC 0230 Manchester United v Inter Milan
International Champions Cup
Jumamosi 02 Agosti 2014, Michigan Stadium, Ann Arbor
2306 Manchester United v Real Madrid
International Champions Cup
Jumanne 12 Agosti 2014, Old Trafford
REUNITED14
2130 Manchester United v Valencia
MFUMO: 3-4-3
Goalkeeper
De Gea
Defenders(Walinzi)
Smalling
Evans
Jones
Midfilders(Viungo)
Valencia
Fletcher(C)
Herrera
Shaw
Attackers(Washambuliaji)
Mata
Welbeck
Rooney
Rooney akifunga goli la pili kwa njia ya penati.
Herrera ameonyesha ni kwanini Manchester United ilikuwa inahitaji huduma yake tangu msimu wa mwaka jana.
Kazi nzuri amefanya. Bila kificho ndio nyota wa mchezo huo.
Aner Herrera akikabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa mechi
Kauli ya Van Gaal baada ya mchezo huo.....
Van Gaal on United's win vs L.AGalaxy :"I dont have to restore theirmentality.They have winners mentality.They just need instructions."
Imeandaliwa na........
Katemi P. Methsela
0 comments:
Post a Comment