Baraza la usalama la Umoja
wa Mataifa limeelezea uhaba wa chakula nchini Sudan Kusini kama mbaya
zaidi kuwahi kuonekana duniani na kuyataka mataifa ambayo yaliahidi
kutoa msaada wa zaidi ya dola millioni mia sita kutoa fedha hizo.
Shirika la chakula duniani WFP limesema kuwa iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa watoto elfu hamsini huenda wakapoteza maisha yao kutokana na utapia mlo mwaka huu huku thuluthi moja ya raia wakikabiliwa na na viwango hatari vya njaa.
0 comments:
Post a Comment