Mzozo umeibuka kwenye Bunge la
India baada ya kuwepo Ripoti kuwa baadhi ya Wabunge wa dini ya Hindu
walijaribu kumshurutisha mtu mmoja aliyekuwa kwenye mfungo wa Ramadhan
kula chakula.
Wabunge hao kutoka mrengo wa kulia wa Chama cha
Shiv Sena wameripotiwa kuwa walikuwa na hasira kwa kuwa hawakupatiwa
chakula walichokichagua katika mgahawa wa Serikali.Vyama vya upinzani vikiongozwa na chama cha Congress wamekemea kitendo hicho wakisema ni ukiukwaji wa imani ya dini,na kutaka chama cha Shiv Sena kuomba radhi.
Kwa mujibu wa Ripoti, tukio hilo lilitokea jumanne mjini Delhi baada ya wabunge kadhaa kutoka chama cha Shiv Sena cha jimbo la Maharashtra kuchukizwa na hali ya kutokuwepo kwa chakula walichokitaka na kutumia nguvu kusokomeza kipande cha mkate mdomoni mwa mfanyakazi wa mgahawa aliyekuwa katika mfungo.
Gazeti la Indian Express limesema baada ya tukio hilo, kazi katika mgahawa huo zilisimama, huku msimamizi wa mgahawa akilalamika kuwa mfanyakazi huyo amesikitishwa sana na kitendo hicho.
Chama cha Shiv Sena kimekana kuhusika kwenye tukio hilo kikidai kuwa njama za kisiasa.
0 comments:
Post a Comment