Chama cha Madaktari nchini
Tanzania kimelaani kitendo cha kutupwa kwa viungo vya binadamu nje ya
jiji la Dar es Salaam kinyume cha sheria.
Rais wa chama hicho, Dk. Primus Saidia ametaka
hatua madhubuti zichukuliwe dhidi ya wahusika ikiwemo kupigwa marufuku
kwa mtu au taasisi iliyohusika kuendesha shughuli zozote za utafiti kwa
kutumia viungo vya binadamu.Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chama hicho cha madaktari hapa jijini Dar es Salaam, kiongozi huyo ametaka hatua madhubuti zikuchuliwe dhidi ya wahusika ikiwemo kufungiwa.
Sakata la kutupwa kwa viungo hivyo kinyume cha sheria katika mji wa Mbweni nje ya jiji la Dar es Salaam siku mbili zilizopita, lilizua taharuki miongoni mwa watu wa kada mbalimbali.
Tayari watu wanane kutoka Chuo cha udaktari cha IMTU kilichopo hapa jijini Dar es Salaam wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuhusishwa kwa kutupwa kwa viungo hivyo ambavyo viliwekwa katika mifuko ya plastiki ipatayo 85.
0 comments:
Post a Comment