Vikosi vya zima moto vya Libya
vinapambana kujaribu kuuzima moto baada ya kombora la roketi kulipua
tanki la kuhifadhia mafuta wakati wa mapigano kati ya makundi mawili
yanayohasimiana katika mji mkuu Tripoli. Tanki hilo ni miongoni mwa
matanki yanayomilikiwa na Kampuni ya mafuta ya serikali ya Libya yenye
lita milioni sita za mafuta.
Msemaji wa Kampuni hiyo Mohamed Al-Hariri amesema iwapo moto huo utasambaa kwenye matanki mengine ya karibu huenda ukasababisha madhara makubwa katika eneo lenye upana wa kilomita tano.
Serikali ya muda ya Libya imetaka ustishaji wa
mapigano katika eneo hilo la maafa ili kuruhusu vikosi vya zima moto
kufanya kazi yao bila kuingiliwa.Msemaji wa Kampuni hiyo Mohamed Al-Hariri amesema iwapo moto huo utasambaa kwenye matanki mengine ya karibu huenda ukasababisha madhara makubwa katika eneo lenye upana wa kilomita tano.
0 comments:
Post a Comment