Facebook

Friday, 25 July 2014

Nigeria kuzungumza na Stephen Keshi

NFF inajadiliana na Keshi kuhusu kandarasi mpya
Shirikisho la kandanda la Nigeria NFF limesema kuwa linaanda mikakati ya kufanya mazungumzo na aliyekuwa kocha wa timu ya taifa Super Eagles Stephen Keshi wakimtaka aendelee kuhudumu kama mkufunzi mkuu.
Kauli hii mpya ni tofauti na ile iliyochukuliwa na afisi iliyokuwepo awali ambayo ilikataa kuandikisha kandarasi upya naye.
Hata hivyo waziri wa michezo wa Nigeria anasemekana hakufurahishwa na matakwa mapya ya nyongeza ya mshahara alioitisha Keshi.
Keshi anasemekana kuwa aliomba kuongezewa mshahara wake maradufu hadi kutimia dola elfu thelathini ($30,000) kwa mwezi na kuwa pesa hizo zilipwe kabla hajaanza hatamu mpya.
Uongozi wake kocha Keshi umekumbwa na migomo ya mara kwa mara kuhusiana na malimbikizi ya marupurupu ya wachezaji na mishaharaa yao.
Keshi hata hivyo anakumbukwa kwa kuingoza The Super Eagles kunyanyua kombe la mabingwa barani Afrika mwaka wa 2013 mbali na kutimu raundi ya pili ya kombe la dunia la mwaka huu lililokamilika huko Brazil mapema mwezi huu.
Maigari Aminu amen'golewa madarakani Nigeria
Kamati kuu ya NFF hata hivyo imeagiza mazungumzo yaanze kwa niya ya kuandikisha upya kandarasi naye katika kipindi cha juma moja lijalo.
Wakati huohuo waziri wa michezo Tammy Danagogo amewaasa wadau wa kandanda nchini humo kuzika tofauti zao na kuimarisha viwango vya kandanda .
Danagogo alisema kuwa maafisa hawana budi kusitisha malumbano na vita vya kungangania uongozi kwa niya ya kujifaidisha .
Waziri aliyasema hayo muda mchache baada ya kamati kuu ya NFF kumn'goa mamlakani mwenyekiti wa shirikisho hilo
Aminu Maigari kwa madai ya ufujaji fedha za shirikisho.
Kamati hiyo ilichukua hatua hiyo takriban juma moja baada ya mapatano kati yao na shirikisho la soka duniani FIFA kumrejesha mamlakani baada ya mahakama moja kumng'oa uongozini.
Makamu wake , Chief Mike Okeke Umeh, ndiye atakayechukua hatamu kama kaimu mwenyekiti wa NFF hadi uchaguzi ujao utakaofanyika Agosti tarehe 26.

0 comments:

Post a Comment