Facebook

Wednesday, 30 July 2014

Tetemeko la Ardhi laitikisa Morogoro.

Leo majira ya saa tisa usiku kumetokea tetemeko la ardhi katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Morogoro,yakiwemo maeneo ya Bigwa,Tungi,Kolla B,Misongeni Lilidumu kwa sekunde chache
sana,ila lilitikisa kweli kweli!mpaka sasa hakuna madhara yaliyoripotiwa kusababishwa na tetemeko hilo.Tunaomba taarifa kamili kutoka kwa vyombo husika.
 

HISTORIA YA TETEMEKO LA ARDHI


MAANA YA TETEMEKO KWA UFUPI
Tetemeko la ardhi(zilizala) ni mishtuko ya ghafla ya ardhi. Inatokea mara kwa mara lakini idadi kubwa ni hafifu mno haisikiki na wanadamu ila tu inapimwa na mitambo ya wataalamu.

SABABU ZA TETEMEKO
Sababu ya tetemeko ni mara nyingi miendo ya gandunia kama kusukumana kwa mabamba ya ganda la dunia . Ili kufahamu sababu hiyo ya matetemeko ya ardhi, inabidi kufahamu mambo yanayoendelea chini ya ardhi.


 Kwanza ni lazima kufikiria xd :Wuundo wa dunia. Dunia ina umbo la duara. Umbali uliopo baina ya pande mbili tofauti kinyume za dunia ni kilomita elfu kumi na tatu. Katika sehemu ya nje ya dunia, ardhi ni thabiti (ngumu). 

Dunia ina gamba la mwamba ngumu ambalo, kulingana na ukubwa wa dunia yenyewe, ni jembamba. Gamba hilo lina unene ya baina kilomita kumi na kilomita hamsini. Kama ungeweza kusafiri chini ya ardhi, yaani kuvuka gamba hilo, ungeona kwamba mazingira ni tofauti sana. Kila kitu kwenye dunia kinavutwa kuelekea sehemu ya kati ya dunia ( graviti). 

Kwa hiyo kuna shinikizo kubwa mno chini ya gamba kutokana na msukumo kwa vitu vya juu kuelekea chini.Yote ni mwamba na chuma, lakini kutokana na shinikizo hilo, kuna joto kali sana, na mwamba na chuma chini ya gamba si imara. Kwa hiyo mwamba wa chuma umeyeyuka, kama matope joto yanayotoka nje ya volkeno wakati wa mlipuko .

Ambapo matope hayo yanapokuwa baridi, yanakuwa imara kama mwamba wa kawaida. Mwamba huo ulioyeyuka wenye joto mno unasogea ukizunguka chini ya gamba. Kwa upande wake, gamba linavutwa pia na mwamba ulioyeyuka, likisogea pia. Kwa sababu ya kusukumwa, gamba huvunjika. Kwa hiyo badala ya pande moja zima la gamba, kuna baadhi ya mapande makubwa ya gamba yanayosogea yakiwa na nguvu kubwa mno. 


HATARI ZA TETEMEKO LA ARDHI
Tetemeko kubwa laweza kusababisha uharibifu mkubwa na vifo hasa kutokana na majengo yanayoanguka. Baharini tetemeko laweza kusababisha tsunami.


Imeandaliwa na......
                               Mdau Wetu

0 comments:

Post a Comment