Habari zilizotufikia hivi punde kutoka kwa ripota wetu aliyeko Musoma-Mara,Mr.Japhet Daudi ni kwamba;
Ajali mbaya sana imetokea eno la Sabasaba,Musoma-Mara.Ajali hiyo imehusisha mabasi mawili;Mwanza Coach na J4 Express yanayofanya safari zake Mwanza-Musoma.Ilikuwa ni majira ya saa 7 mchana wa leo.
Chanzo cha ajali hiyo ni kutokana mwendo kasi wa mabasi hayo kwani ajali iliyosababishwa na kugongana kwa mabasi hayo uso kwa uso katika eneo la darajani,Sababa-Musoma.
Ripota wetu anaeleza kwamba magari hayo yote yalikuwa katika mwendokasi na sehemu yalipokuwa ni darajani na daraja hilo linauwezo wa kupitisha gari moja tu,kutokana na spidi ya mabasi hayo mojamoja yalijikuta yakishindwa kupishana kutokana na udogo wa daraja hili na hivyo kusababisha ajali mbaya sana ambayo mabasi hayo mawili yaligongana uso kwa uso.
Na ukiachana na mwendo kasi wa mabasi hayo,pia eneo hilo kuna mteremko mkali kabla haujafikia sehemu ya daraja hilo na mabasi yote yalikuwa yanawahi kuvuka sehemu hiyo.
Madereva wa mabasi yote mawili walifariki papo hapo huku hadi hivi sasa inasemekana ni watu zaidi ya 60 walipoteza maisha papo hapo.Huku wengine wakikatika viungo mbalimbi vya miili yao kama vile miguu,mikono.Tayari polisi wamefika eneo hilo na kuikusanya miili yote kwa ajili ya taratibu nyingine.
Endelea kutembelea www.bantutz.com tutakujuza kila kitakachokuwa kinaendelea.BantuTz inakuletea taarifa zote kwa muda na wakati muafaka.
Source:Japhet David {BantuTz RIPORTER-MUSOMA}
{0753 035717}
Imeandaliwa na............................
Katemi Methsela
{C.E.O BantuTz }
0 comments:
Post a Comment