Baraza la Tiba za Asili na Tiba
Mbadala Tanzania limesitisha vibali vya kurusha matangazo ya tiba za
asili na mbadala kwenye vyombo vyote vya habari kwa kile kilichoelezwa
kuwa yanapotosha jamii.
Taarifa iliyotolewa na kwa vyombo vya habari ,
imeeleza kuwa katika siku za karibuni kumekuwapo na matangazo mbalimbali
ya tiba hizo ambayo baadhi yake hayaisaidii jamii.Kutokana na taarifa hiyo ya baraza, vyombo vya habari havipaswi kupokea kibali chochote cha kutangaza matangazo ya tiba hizo hivi sasa, kwa kuwa ni batili.
Pia taarifa hiyo inaeleza kuwa, chombo chochote kitakachorusha tangazo au kipindi kitatozwa faini na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Naye mtaalam wa tiba asili, tabibu Rahabu Rubago amesema kuwa hatua hiyo ya Baraza imetolewa bila wao kupatiwa taarifa hiyo mapema na kueleza kuwa watapata hasara kwa kuwa baadhi yao wametengeneza vipindi tayari kwa ajili ya kuvirusha kwenye vyombo vya habari.
0 comments:
Post a Comment