Facebook

Tuesday, 19 May 2015

AYEW ATWAA TUZO UFARANSA

KIUNGO wa kimataifa wa Ghana, Andre Ayew ameteuliwa kuwa
mchezaji bora kutoka Afrika anayecheza katika Ligi Kuu ya
Ufaransa leo.
Ayew amemaliza akiwa kinara akiwazidi Max-Alain Gradel wa Ivory
Coast na klabu ya Saint-Etinne na Aymen Abdennour kutoka Tunisia
anayekipiga katika timu ya Monaco.
Kiungo huyo amekuwa katika kiwango kikubwa msimu huu na kuzivutia
klabu mbalimbali nchini Uingereza zikiwemo Liverpool, Tottenham
Hotspurs, Arsenal na hata Newcastle United ambao wako katika
hatari ya kushuka daraja.
Ayew ambaye amekuwa na Marseille kipindi cha miaka 10, alitangaza
mapema kuwa msimu huu ndio utakuwa wa mwisho kwake kuitumikia
timu hiyo.

Related Posts:

  • Yanga vs Azam Pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara linafunguliwa leo kwa mchezo wa Ngao ya Jamii kwa wakali wa Jangwani Yanga SC kucheza na timu ya Azam FC, Uwanja wa Taifa kuanzia majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Masharik… Read More
  • KIKOSI CHA AZAM FC DHIDI YANGA1. MWADINI ALI 2. SHOMARI KAPOMBE 3. ERASTO NYONI 4. DAVID MWANTIKA 5. AGGREY MORIS 6. BOLOU MICHAEL 7. HIMIDI MAO 8. SALUM ABUBAKAR 9. DIDIER KAVUMBAGU 10. KIPRE TCHETCHE 11. LEONEL SAINT PREUX AKIBA AISHI MANULA MUDATHIR YA… Read More
  • RATIBA ULAYA | UEFA Champions LeagueLeo Jumanne 21:45 Olympiakos Piraeus vs Atlético Madrid 21:45 Juventus vs Malmö FF 21:45 Liverpool vs Ludogorets 21:45 Real Madrid vs Basel 21:45 Monaco vs Bayer Leverkusen 21:45 Benfica vs Zenit 21:45 Galatasaray v… Read More
  • Ligi Kuu Uingereza:Arsenal kukumbana na Manchester City hapo kesho.Uwanja-Emiraters Mashabiki-60,300 Timu-Arsenal vs man city Arsenal ni timu iliyoanzishwa mwaka 1889 kaskazini mwa jiji LA London Mpaka sasa Arsenal wamekutana Na man city mara184 ~Arsenal wameshinda Mara 93 ~Manchester city a… Read More
  • Diego Costa mchezaji bora Ligi kuu Uingereza.Diego Costa ameshinda tuzo ya mchezaji bora Premier League kwa mwezi August kwa kuwapiku Cesc Fabregas (Chelsea), Nathan Dyer (Swansea),Gylfi Sigurdsson (Swansea) na Andreas Weimann (Aston Villa). Mourinho ambaye ndiye anayek… Read More

0 comments:

Post a Comment