Hapo jana BantuTZ.com tuliripoti kuhusiana na mgomo wa wanafunzi wa Chuo Kikuu hapo jama usiku kwa wale wanaoishi 'Mabibo Hostel'.
Lakini muda huu mgomo huo umehamia katika eneo la Chuo Kikuu Cha DSM.
Matamko ya viongozi wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu DSM "Daruso" ni kuwa kwa siku ya leo wanafunzi watabaki ndani ya eneo ya Chuo yaani "main campus" mpaka pesa za kujikimu 'BOOM' zitakapoingia kwenye akaunti za wanafunzi.
Pili ni wanafunzi wamesema hawataondoka mpaka hela za masomo kwa vitendo 'field' watakapopewa wakiwa chuoni.
Jambo la tatu ni kuwa wanafunzi wa Chuo Kikuu DSM wanaitaka serikali ipandishe fedha ya kujikimu kama ambavyo ilitoa ahadi mwaka 2010 hivyo wanafunzi wanaitaka serikali kupitia Waziri Mkuu kuitekeleza ahadi hiyo kwa sababu gharama ya maisha imepanda.
Taarifa tulioipata kutoka kwa ripota wa BantuTz Chuo Kikuu DSM ni kwamba hata kupiga picha imekatazwa kaka ili kulinda wale wanaongea kwani kuna mtindo picha hutumka kufukuzisha wanafunzi hivyo basi waandishi wahabari tu ndo wameruhusiwa kupiga picha na kuchukua picha za tukio.
Polisi pia wapo wanalinda amami lakini hawana tatizo na wanafunzi,ofisi za utawala wa Chuo zinalindwa pamoja na vunga vyote vya Chuo.Masomo hakuna polisi wanachofanya ni kuimarisha doria tu.
Endelea kutembelea www.bantutz.com kwa habari za kina na uhakika.
0 comments:
Post a Comment