Facebook

Monday, 18 May 2015

Wanafunzi wa Chuo Kikuu DSM wanaokaa Mabibo Hostel waamua kugoma baada ya kucheleweshewa pesa za kujikimu "Boom"

BantuTz BREAKING NEWS

Habari zilizotufikia BantuTz.com hivi punde ni kwamba wanafunzi wa chuo kikuu Dsm wanaoishi mabibo hostel wameamua kuandamana kisa kikiwa ni kucheleweshewa pesa zao za kujikimu kutoka kwa serikali.

Sakata hili limeibuka baada ya serikali ya wanafunzi pamoja na chuo kutoa tangazo na kuujulisha umaa kuwa wanafunz zaidi ya elfu 6 wamekosa mkopo kutokana na ucheleweshwaji wa fedha hivyo waliobahatika kupata ni wanafunzi 4100 tu (divide and rule)

Sasa wanafunzi wampatwa na hasira walipoambiwa watakopeshwa sh elfu ishirin iwasaidie mpaka watakapo pewa fedha zao.

Lazima tuelewe kuna wanafunzi bila 'boom' maisha yao hayaendi hakuna mtu anayependa kugoma kisa laki nne na nusu ila uwezo wa kijikimu umewawia vigumu hawana namna yoyote ya kuoata pesa.

Chuo cha DIT walipewa 'BOOM' Ijumaa iliyopita, Huku wanafunzi waliopewa BOOM Chuo kikuu DSM Ni wale wa CoET, CoNAS na CoICT.
----------------------------------------

Hii ndio taarifa iliyotolewa na Uongozi wa serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu DSM (DARUSO)

CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

SERIKALI YA WANAFUNZI (DARUSO)

TAARIFA KWA WANADARUSO KUHUSU KUCHELEWA KWA FEDHA YA KUJIKIMU KWA BAADHI YA VITIVO

Ndugu Wanadaruso;

Kama tangazo la tarehe 7/5/2015 kupitia Wizara ya Mikopo lilivyosema, Serikali ya Daruso tukishirikiana na Menejimenti ya Chuo tulifanya jitihada ya kuhakikisha tunapata fedha hizo kwa wakati, lakini fedha iliyotolewa mpaka sasa ni kwa wanafunzi 4100 na waliosalia ni 6120.  Tulipewa taarifa kuwa wangeweza kuingiziwa fedha hizo Jumatatu ya leo tarehe 18/5/2015 lakini hadi kufikia jioni ya leo fedha hizo hazijafika kwenye akaunti ya chuo kama ilivyotarajiwa.

Hivyo basi, serikali ya Daruso tumeomba Menejimenti ya Chuo kuazimisha fedha ya kujikimu kwa wanafunzi ili kuweza kutuokoa katika kipindi hiki kigumu tukiwa tunaendelea na mchakato wa ufuatiliaji wa fedha ya kujikimu kutoka Bodi ya Mikopo.

Uongozi wa Chuo umekubali ombi hilo hivyo tunawataarifu wana Daruso kuwa kuanzia tarehe 19/5/2015 (kesho) saa sita mchana kutakuwa na zoezi la kusaini fomu maalum za kuazimishwa fedha za kujikimu kwa siku tano kiasi cha shilingi 20,000/= (elfu ishirini) taslimu na fedha hizo zitatolewa bila riba siku ya Jumatano kwa watakoridhia.

NB:
Ufuatiliaji wa fedha za kujikimu unaendelea na taarifa itatolewa kwa kila hatua tutakayofikia.


NAKALA:

Prof. D.A.
Mfinanga Naibu Makamu Mkuu wa Chuo - Utawala
-----------------------------------------
Endelea kutembelea www.bantutz.com kwa habari za kina na uhakika.

0 comments:

Post a Comment