Facebook

Tuesday, 12 May 2015

UCHAMBUZI:Nusu Fainali 2 Bayern Munchen vs Barcelona Je The Bavarians wanawezeza kugeuza ubao leo? Ungana hapa na Mr Choi.

Katika usiku wa barani Ulaya kwenye michuano ya kombe la mabingwa Uefa pale nchini Ujerumani tuta shuhudia mtanange ktk dimba lenye kuchukua watazamaji 75,000 Allianz Arena kwa vijana wa Pep Guardiola dhidi ya Barcelona.

    Katika mchezo wa awamu ya kwanza viunga vya Catalunya Camp Nou Bayern iliondoka vichwa chini kwa kupokea kichapo cha magoli 3-0 wafungaji wakiwa Messi alie pachika mawili na Neymar Jr.

    Msimu wa 2012/13 Bavarian ya Jupp Heynckes dimba la Camp Nou Barca walifungwa 3-0 na mchezo ulio fanyika Allianz Arena vijana wa Catalunya wakachezea kichapo cha 4-0 mjumuisho ikawa 7-0 .

     Hivyo kisasi cha goli 3 kilisha rudishwa bado cha goli 4 kumbuka katika msimu huu Bayern hawajapoteza mchezo hata mmoja ktk dimba lao la nyumbani huku wakiwa na uwiano wa kufunga goli zaidi ya moja kwenye dakika 361 kazi ipo kweli na kwa kuangazia michezo miwili iliyo pita hatua 16 bora na robo fainal hapo Allianz Arena Bavarian walitoa kichapo kwa Shaktar Donesk na Fc Porto kwa jumla ya goli 13 .

    Na endapo vijana wa Luis Enrique wataibuka na ushindi usiku wa leo itakuwa ni historia kwa upande wao kwani hawajawai ondoka na ushindi kwenye uwanja wenye mvuto na taswira ya taili Allianz Arena.

    Timu hizi zimekutana mara tisa na kati ya hizo Bayern wameondoka na ushindi mara tano dhidi ya mbili za Barcelona na kutoshana sare michezo miwili.

   Kupoteza kwao kwenye nusu fainal hii dhidi ya Barca itakuwa rekodi kwa upande wao kupoteza nusu fainali mbili mfululizo kwani msimu uliopita walipoteza dhidi ya Real Madrid.
 
     Barcelona mpaka sasa wamecheza dakika 638 pasipo kuruhusu wavu wao kuguswa na mara ya mwisho ilikuwa April 15 kwa goli la kujifunga la Mathieu dhidi ya Psg waki ibuka na ushindi wa 3-1.

       Ni mchezo wa 101 kwa Lionel Messi kwenye michuano ya Ulaya huku ukiwa wa 98 kombe la mabingwa ni kinara wa ufungaji msimu huu akiwa na magoli 10 na 77 kama mfungaji wa muda wote Uefa pia mpaka sasa amepiga pasi timilifu 618 ndani ya dakika 967 kwenye michezo 11.

    Kumbuka mpaka sasa ktk michuano hii MSN wamesha piga mashuti yalio lenga goli 52 kati ya mashuti 1135 kwenye michuano hii huku tukishuhudia magoli 350.

    Jicho jingine ni upande wa mzaliwa wa Terrassa Uhispania mnamo 1980 namzungumzia Xavi Hernandez akicheza atakuwa anafikisha mchezo wa 150 na kuwa rekodi ya Michuano hiyo.
  
    Kabla ya mchezo wa leo takwimu za matokeo kwenye mashindano mbalimbali kwa timu zote:-

         BAYERN-WWLLLL
         BARCA-WWWWW

     Upande wa Barca hakuna majeraha na tutaraji kikosi kilicho cheza mchezo wa awamu ya kwanza upande wa Guardiola ataendelea kukosa huduma za Robben,Ribery,Alaba na Badstuber kama ilivyo kuwa mchezo wa awamu ya kwanza.

     Kukosekana kwao ni pengo hususani kwa Robben mtu ambae ni mzuri kwa kulazimisha mashambulizi akitumia vyema unyumbulifu wake na ukiangazia mchezo wa awamu ya kwanza Bayern walimiliki mpira vyema isipo kuwa waka kosa ubunifu wa mtu kama Robben kwenye zone ya Barca.

    Kuwazui Barca si kazi kama kumzuia Messi kufunga au kupitisha mipira yake hatari, goli la tatu Camp Nou walifungwa kutokana na kujitoa muhanga kwa kutafuta goli 1 la ugenini kisha wakafa kwa kaunta hivyo siku ya leo licha ya kutafuta magoli 4 na pengine tukitaraji wao kuanza kwa spidi sana kama ilivyo kuwa kwa Porto wasisahau kuna utofauti wa Porto na Barca kwenye zone zote ndani ya uwanja hivyo kufunguka kwao kwa kupitiliza kutakuwa ni mwanya kwa MSN kombinesheni bora msimu huu kuwajeruhi.

   Laiti uwepo wa kina Robben ungekuwepo ungempa nafuu Guardiola ya ufikiri wa mchezo hata kwa mashabiki pia ila tatizo ubunifu wa waliopo ni wakawaida sana mbele ya Barca.

    Cha msingi ni kuwa na utulivu wa kukaba nafasi wajitahidi umiliki wa mpira uwe upande wao na wapeleke mashambulizi hatarishi zone ya Barca ( mipira mirefu) pasipo kuweka mianya kwenye safu ya ulinzi kuzuia kaunta.

    Gotze anaeshika nafasi ya tatu kwenye orodha ya wachezaji wanao piga pasi timilifu ( 380) ataongoza jahazi kwa kusaidiana na kina Muller,Lewandowski na chagizo la kiungo bora Thiago tukutane majira ya 21:45 pindi mwamuzi Martin Clattenburg atakapo puliza kipenga.

For more/ Ushauri::
Choikangta.ckt@gmail.com

0 comments:

Post a Comment