Mshambuliaji wa Zamalek Dominque da Sila amefungiwa na shirikisho la Soka la Afrika Caf kwa kumpiga mwamuzi. Tukio hilo lilitokea katika mechi ya Champions League kati ya Zamalek dhidi ya TP Mazembe tarehe 8 Juni 2014 mjini Lubumbashi.
Caf imesema Da Silva alikatisha uwanja
mzima baada ya mchezo kumalizika ili kumpiga mwamuzi. Wachezaji wengine
wa Zamalek, Abdelrehim Mahmoud na Hazem Mohamed Emam pia wamefungiwa
mechi moja kila mmoja kwa kuhusika na vurugu hizo.
Da Silva atakosa
michezo mitatu ya kimataifa: wa marudio na TP Mazembe, na wa AS Vita na
dhidi ya Al Hilal. Pia amepigwa faini ya dola 5,000. Mahmoud atakosa
mchezo dhidi ya TP Mazembe, huku Emam atakosa mchezo dhidi ya AS Vita.
Wawili hao wamepigwa faini ya dola 3,000.
0 comments:
Post a Comment