
Arsenal imemsaini Fulbeki Mathieu Debuchy kutoka Newcastle.
Debuchy, Miaka 28, alikuwa mmoja wa Wachezaji wa France waliocheza Kombe la Dunia huko Brazil na ameletwa Emirates kuchukua nafasi ya Bacary Sagna ambae amejiunga na Manchester City kama Mchezaji Huru.

Debuchy, ambae ameigharimu Arsenal Pauni Milioni 12, anakuwa Mchezaji wa Pili kusainiwa na Arsenal kwa Msimu mpya baada kumchukua Alexis Sánchez kutoka Barcelona.

Mfaransa huyo aliichezea Newcastle Mechi 46 katika Miezi 18 aliyokuwa kuwa huko baada kuhamia kutoka Lille ya France ambayo alifanikiwa kutwaa nayo Ubingwa wa Ligue 1 na Coupe de France Msimu wa 2010/11.
JANMAAT ASAINI NEWCASTLE
Newcastle United wamemsaini Fulbeki wa Kimataifa wa Netherlands Daryl Janmaat kutoka Feyenoord kwa Dau ambalo halikutajwa.
Janmaat, Miaka 24, amesaini Mkataba wa Miaka 6 na amenunuliwa ili kuziba pengo la Mathieu Debuchy aliehamia Arsenal
Janmaat aliichezea Netherlands Mechi 5 huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia na kufika nayo Nusu Fainali.
Mdachi huyo alianzia Soka lake huko ADO Den Haag kisha kujiunga na Heerenveen Mwaka 2008 ambako alicheza Mechi zaidi ya 100 kabla kujiunga na Feyenoord Mwaka 2012.
0 comments:
Post a Comment