Kampuni ya upili kwa ukubwa
katika utengenezaji wa sigara nchini Marekani imeagizwa kulipa kitita
kikubwa cha dola billioni 23 kwa mke wa mwathiriwa mmoja wa sigara
aliyefariki kutokana na saratani ya mapafu.
Mjane huyo Cynthia Robinson alichukua hatua
dhidi ya kampuni ya sigara ya R.J Reynolds baada ya kifo cha mumewe
aliyekuwa na miaka 36.Kampuni hiyo imeyataja malipo hayo kama yasio na haki na kusema kuwa itakata rufaa.
Wakili wa bi Robinson amesema kuwa kampuni hiyo ya sigara iliuza sigara hizo bila kutoa tahadhari yoyote kuhusu tishio la uvutaji wake.
0 comments:
Post a Comment