
Demba Ba sasa kuvaa jesi ya Besiktas ya Uturuki
Usajili mpya na mikataba mipya kwa wachezaji vinara ndio shughuli kuu inayoendelea sasa kabla msimu mpya wa michuano kuanza..
Pamoja na kasheshe zinazomuandama, Suarez sasa
yuko Bacelona 100% baada ya kuihama Liverpool, nae Demba Ba tayari
amewasili Uturuki anakotarajiwa kukamilisha uhamiaji wake kutoka Chelsea
hadi Besiktas kwa gharama ya £8m.Demba Ba amewahi kuifungia Chelsea angalau mabao 14.
Hivyo Chelsea wamejibu kwa kumshawishi Filipe Luis aihame Atletico Madrid ingaje Mbrazil huyo yuko katika safu ya ulinzi.
Msimu uliopita Luis alishiriki mechi zaidi ya 40 na kilele ikawa Atletico kushinda la liga kwa mara ya kwanza tangu 1996 na pia wakafikia fainali ya Champions League.
0 comments:
Post a Comment