Israel imerejea mashambulio yake ya anga kuelekea Gaza baada ya kusimamisha mapigano kwa muda mfupi.
Awali Israel ilikubali mapendekezo ya Misri ya kusitisha mapigano, na ilisimamisha shughuli zake Jumanne asubuhi.
Awali Israel ilikubali mapendekezo ya Misri ya kusitisha mapigano, na ilisimamisha shughuli zake Jumanne asubuhi.
Hata hivyo, tawi la kijeshi la Hamas, linalodhibiti Gaza lilitupilia mbali pendekezo hilo, likisema kuwa ni kama "kujisalimisha".
Maafisa wa Palestina wanasema watu 192 wameuawa kwa mashambulio ya anga ya Israel, yaliyoanza siku nane zilizopita, ili kuzuia maroketi yanayorushwa kutoka Gaza.
Waisrael wasipopungua wanne wamejeruhiwa vibaya tangu ghasia hizo kuanza, lakini hakuna aliyeuawa.
0 comments:
Post a Comment