Facebook

Tuesday, 8 July 2014

Louis Van Gaal aongeza kocha mwingine kwenye benchi lake la ufundi.

 Photo: LOUIS VAN GAAL AONGEZA KOCHA MWENGINE KWENYE BENCHI LA UFUNDI. 

Louis Van Gaal amemuongeza kocha wa team ya taifa ya vijana ya Uholanzi U-21 katika benchi la ufundi la Manchester United. 

Albert Stuivenberg atakua kocha wa tatu wa kiuholanzi kujiunga kuifundisha Manchester United chini ya utawala wa Louis Van Gaal. Kocha uyo ataungana na Marcel Bout ambaye ana utaalamu wa kuwasoma wapinzani pamoja na Frans Hoek ambaye ana kipaji cha kufundisha makipa. 

Albert Stuivenberg mwenye umri wa miaka 43 atakua kama kocha msaidizi pembeni ya Ryan Giggs ambaye yeye kimsingi atakua msaidizi mkuu. Albert alitumia miaka 7 tangu akiwa na umri wa miaka 36 kuwanoa vijana wenye chini ya umri wa miaka 17 na kufanikiwa kuchukua ubingwa wa ulaya mwaka 2011 na 2012. 

Stuivernberg alianza mafanikio yake katika klabu ya Fayenoord kabla ya kuitwa na taifa lake kuitumikia team ya taifa ya vijana wenye umri wa miaka 21 ambapo ujuzi wake na umahiri mkubwa umemfanya kuchaguliwa na Manager mpya Louis van Gaal. Anataraji kujiunga na Ryan Giggs haraka iwezekanavyo baada ya uteuzi huu kukamilika. 

#KaribuAlbert 

=/ D.P /=
Louis Van Gaal amemuongeza kocha wa team ya taifa ya vijana ya Uholanzi U-21 katika benchi la ufundi la Manchester United.

Albert Stuivenberg atakua kocha wa tatu wa kiuholanzi kujiunga kuifundisha Manchester United chini ya utawala wa Louis Van Gaal. Kocha huyo ataungana na Marcel Bout ambaye ana utaalamu wa kuwasoma wapinzani pamoja na Frans Hoek ambaye ana kipaji cha kufundisha makipa.

Albert Stuivenberg mwenye umri wa miaka 43 atakua kama kocha msaidizi pembeni ya Ryan Giggs ambaye yeye kimsingi atakua msaidizi mkuu. Albert alitumia miaka 7 tangu akiwa na umri wa miaka 36 kuwanoa vijana wenye chini ya umri wa miaka 17 na kufanikiwa kuchukua ubingwa wa ulaya mwaka 2011 na 2012.

Stuivernberg alianza mafanikio yake katika klabu ya Fayenoord kabla ya kuitwa na taifa lake kuitumikia team ya taifa ya vijana wenye umri wa miaka 21 ambapo ujuzi wake na umahiri mkubwa umemfanya kuchaguliwa na kocha mpya Louis van Gaal. Anataraji kujiunga na Ryan Giggs haraka iwezekanavyo baada ya uteuzi huu kukamilika. 

   Imeandaliwa na....
                                 James Nicholaus

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment