Facebook

Sunday, 20 July 2014

Taifa Stars yajiweka katika nafasi mbaya kufuzu fainali za Mataifa Huru ya Afrika.


Photo: Matokeo- Kombe la Mataifa Afrika
Tanzania 2-2 Msumbiji

  Taifa Stars leo wamejiweka pagumu kufuzu kuingia Hatua ya Makundi ya kusaka nafasi za kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, huko Morocco Mwakani, baada kutoka Sare 2-2 na Msumbiji kwenye Mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Stars, wakiwa chini ya Kocha Mart Nooij ambae kati ya Mwaka 2007 na 2011 alikuwa Kocha wa Msumbiji, walitanguliwa kufungwa kwa Bao la Penati iliyopigwa na Domingues lakini walijitutumua na kusawazisha kwa Bao la Mcha Khamis ambae pia alifunga Bao la Pili kwa Penati.

Hata hivyo, kazi hiyo njema ilipotea bure baada ya kuwaruhusu Msumbiji kusawazisha katika Dakika ya 89 kwa Bao la Isaac Carvalho.

MAGOLI:
Tanzania 2
-Mcha Khamis Dakika ya 66 & 71 [Penati]
Mozambique 2
-Gaspar Domingues Dakika ya 48 [Penati]
-Isac Carvalho 89
Photo: Matokeo Kombe la Mataifa ya Afrika
Photo: Matokeo Kombe la Mataifa ya Afrika
Kwenye Marudiano huko Maputo, Msumbiji, Tanzania wanahitaji ushindi au Sare ya Bao 3-3 na kuendelea.
Kwenye Mechi nyingine iliyochezwa Leo huko Setsoto Stadium, Maseru, Wenyeji Lesotho waliifunga Kenya Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 70 la Moletsane.
Mechi za Marudiano zitachezwa Wikiendi ya Agosti 1 hadi 3.

AFCON 2015-MOROCCO
RATIBA/MATOKEO:

Jumamosi Julai 19
Uganda 2-0 Equatorial Guinea 
Botswana 2-0 Guinea-Bissau 
Sierra Leone 2-0 Seychelles 

Jumapili Julai 20
Lesotho 1-0 Kenya 
Tanzania 2-2 Mozambique 

17:30 Congo v Rwanda
18:00 Benin v Malawi

Mechi za Marudiano zitachezwa Wikiendi ya Agosti 1 hadi 3.
MAKUNDI:

KUNDI A
-Nigeria
-South Africa
-Sudan
-Mshindi Congo/Rwanda

KUNDI B
-Mali
-Algeria
-Ethiopia
Mshindi Benin/Malawi

KUNDI C
-Burkina Faso
-Angola
-Gabon
-Mshindi Lesotho/Kenya

KUNDI D
-Ivory Coast
-Cameroun
-Congo DR
-Mshindi Sierra Leone/Seychelles

KUNDI E
-Ghana
-Togo
-Guinea
Mshindi Uganda/Mauritania

KUNDI F
-Zambia
-Cape Verde
-Niger
-Mshindi Tanzania/Msumbiji

KUNDI G
-Tunisia
-Egypt
-Senegal
-Mshindi Botswana/Guinea-Bissau

0 comments:

Post a Comment