TETESI ZA SOKA ULAYA

Kocha mpya wa Manchester United Louis van Gaal angependa kumchukua Wesley Sneijder, 30, kutoka Galatasaray, lakini klabu hiyo ya Uturuki inataka pauni takriban milioni 6 (Sun),

Kocha mpya wa Manchester United Louis van Gaal angependa kumchukua Wesley Sneijder, 30, kutoka Galatasaray, lakini klabu hiyo ya Uturuki inataka pauni takriban milioni 6 (Sun),
Liverpool watamuuza Luis Suarez,
27, kwenda Barcelona mwisho wa wiki
hii, ikiwa klabu hizo zitakubaliana ada ya pauni milioni 75 (Daily
Mirror),
Lakini Arsenal wamekasirishwa kwa sababu jaribio lao la
kumchukua Alexis Sanchez, 25, kutoka Barcelona linacheleweshwa kutokana
na mkataba wa Suarez kudemadema (Daily Express),
Arsenal wanataka
kulipwa pauni milioni 6 kumuuza Mikel Arteta, 32, kwenda Fiorentina
(Times),
Roma wamewapa Manchester City hadi tarehe 21 mwezi huu wawe
wamekamilisha usajili wa beki wa kati kutoka Morrocco Mehdi Benatia, 27,
(Guardian),
Chelsea wanamsajili beki wa kulia wa Atletico Madrid, Luis
Filipe, 28, kuziba nafasi ya Ashley Cole aliyekwenda Roma (Sun),
Winga
kutoka Colombia Juan Cuadrado, 27, huenda akahamia Manchester United
kutoka Fiorentina (London Evening Standard),
Mshambuliaji wa Liverpool
Iago Aspas, 26, anajiandaa kuhamia Sevilla, baada ya kushindwa kupata
namba Anfield (Daily Star),
Brendan Rodgers pia anafikia kutoa pauni
milioni 10 kumchukua beki wa kushoto wa Swansea Ben Davies, 21 (Daily
Telegraph),
Manchester United, Liverpool, Chelsea na Arsenal zitapambana
kupata saini ya winga wa Benfica Joao Filipe anayetajwa kuwa "Cristiano
Ronaldo mwingine" pamoja na kipa Joao Virginia, wote wana umri wa miaka
15 (Daily Express),
Manchester United wanafikiria kumsajili beki wa
kushoto wa Wolfsburg na Uswisi, Ricardo Rodriguez, 21, kuziba nafasi ya
Patrice Evra ambaye huenda akahamia Juventus (Times),
Lakini Louis van
Gaal pia huenda akamchukua beki Daley Blind, 24, kutoka Feyenoord ikiwa
Evra ataondoka (Manchester Evening News),
kiungo kutoka Nigeria Michael
Babatunde, 21, anayechezea Volyn Lutsk nchini Ukraine, amedai kuwa
Sunderland wanataka kumsajili (Newcastle Chronicle),
Bayern Munich
wamesema wamefikia makubaliano yasiyo ya maandishi na Atletico Madrid ya
kumsajili Mario Mandzukic, 28 (Marca),
Mshambuliaji wa Real Madrid
Alvaro Morata huenda akajiunga na Juventus mapema wiki ijayo
(Tuttosport),
Hatimaye, kinyozi wa Alexis Sanchez amethibitisha kuwa
mchezaji huyo anahamia Arsenal! (Metro).
Share tetesi hizi na wapenzi
wote wa soka. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Cheers!
0 comments:
Post a Comment