Facebook

Sunday, 20 July 2014

Walcott azidi kupata majanga.

 Photo: WALCOTT KUKOSA MWANZO WA MSIMU
Mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott atakosa mechi za mwanzo za msimu wa Ligi Kuu ya England kutokana na jeraha la goti, lakini huenda akaanza mazoezi mwishoni mwa mwezi Agosti.
Walcott, 25, aliumia goti la kushoto katika mchezo wa raundi ya tatu ya Kombe la FA dhidi ya Tottenham mwezi Januari.
"Tunatarajia atarejea mazoezini kikamilifu mwishoni mwa Agosti," amesema meneja wa Arsenal, Arsene Wenger.
"Theo ana msingi mzuri wa matibabu, ambao anautimia sasa," amesema Wenger ambaye pia amesema Walcott atarejea "haraka sana" kucheza mechi mara tu atakapoanza mazoezi.
Walcott alipoumia, Arsenal ilisema hatocheza kwa karibu miezi sita. Hata hivyo klabu hiyo sasa imekiri kuwa hatoweza kurudi kabla ya kuanza kwa msimu unaoanza Agosti 16.

0 comments:

Post a Comment