Raisi Jakaya Kikwete amesisitiza nia ya Serikali kutumia wahitimu wake wa
vyuo vikuu, kufundisha shule za msingi huku akiwaweka sawa kwa kuwaambia kufanya hivyo si kuwashushia hadhi.
Hatua hiyo ya walimu wenye Shahada kuanza kufundisha shule za msingi tofauti na ilivyozoeleka, chini ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995, ni sehemu ya mageuzi makubwa, yanayotarajiwa kufanyika katika sekta ya elimu nchini. Rais Kikwete alishawahi kutamka mpango huo wa kutumia wasomi wa vyuo vikuu katika shule za msingi, kutokana na idadi kubwa ya wahitimu wa ualimu, kutarajiwa kuwa kwenye soko la ajira. Alisisitiza kuwa baada ya mwaka, wahitimu wa vyuo vikuu watafundisha katika shule hizo na kwamba kufanya hivyo si kuwashushia hadhi.
Akihutubia wananchi mjini Mbinga, kabla ya kufungua kituo cha mabasi na barabara ya Peramiho- Mbinga yenye urefu wa kilometa 78, Kikwete alisema barani Ulaya, hata walimu wa shule za chekechekea wana Shahada na kwamba hicho ni kipimo cha maendeleo. Kwa utaratibu uliozoeleka chini ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995, walimu wa shule za msingi ni wenye cheti.
Hata hivyo, kulingana na taarifa za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, wapo wanaochukua Shahada, wanaosomea kufundisha elimu ya
msingi.
“Wakati umebadilika…leo utamchukua Standard Seven ( Darasa za Saba) kwenda chuo cha ualimu? Leo Division
Four (waliopata Daraja la Nne)
wanakataliwa vyuo vya ualimu,” alisema.
Alisema, hali ya sasa ni tofauti na miaka ya nyuma kwa kuwa sasa, hata makatibu tarafa wana Shahada. Kwa mujibu wa tamko la Serikali, kuanzia sasa wanaosomea ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada, sharti wawe na ufaulu wa daraja la tatu. Aidha, Serikali imeamua kuanzia sasa wanaojiunga na mafunzo ya Stashahada ya Ualimu katika masomo ya Sayansi wakiwa na ufaulu wa Daraja la Kwanza, watasomeshwa bure. Pia
wenye ufaulu wa Daraja la Pili na la Tatu, watapewa mkopo.
0 comments:
Post a Comment