Taarifa
ikufikie kutoka Samukawa, Kanagawa Japan ambako stori kubwa leo
ni kampuni ya Nissan kupata furaha kubwa baada ya kufanikiwa kwa jaribio
la gari walilolitengeneza ambalo linajiendesha lenyewe.
Unaambiwa
limetembea umbali wa kilometa 2.3 likijaribiwa kwenye mikikimikiki ya
aina mbalimbali barabarani kama vile kuovertake, kufata alama za
barabarani, taa za kuongozea magari na hata sehemu za watu kuvuka
barabara.Nissan
wamesema wanalengo la kuanza kuliuza hili gari miaka saba kutoka sasa,
hiyo itakua mwaka 2020 ambapo gari hili lina kamera maalum pamoja na sensors zinazofanikisha
kulipa taarifa ya tukio husika kwa wakati huo ndio maana linaweza
kufanya kama inavyotakiwa mfano kushika breki, kukanyaga mafuta na vitu
vingine.
0 comments:
Post a Comment