Manchester City wameacha kumfuatilia
kiungo wa Everton Ross Barkley, 20, baada
ya kuambiwa atagharimu pauni zisizopungua
milioni 50 (Mirror),
Manchester United
wanakaribia kumsajili winga wa Real Madrid
Angel Di Maria, 26, na huenda atavunja
rekodi ya uhamisho ya Uingereza kwa
mkataba wa pauni milioni 56 (Sky sports),
Manchester United pia wamepanda dau kwa
mara ya pili kumwania kiungo wa Juventus
Arturo Vidal, 27, katika mkataba
utakaohusisha Man U kutoa na mchezaji
(Star),
Mario Balotelli, 24, huenda akawa
mchezaji kamili wa Liverpool katika mkataba
wa pauni milioni 16 ifikapo Jumatatu, lakini
Liverpool wameacha kumfuatilia
mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Samuel
Eto'o, 33, (Liverpool Echo),
Eto'o anadhaniwa
kudai mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki
kutoka kwa Liverpool, lakini sasa inaripotiwa
kuwa anafanya mazungumzo na Everton
ingawa kuna timu za Mashariki ya Kati pia
zinamtaka (Mirror),
Balotelli hatosaini
mkataba wenye kipengele cha utovu wa
nidhamu. Mwakilishi wa mshambuliaji huyo
Mino Raiola amedai kuwa mkataba huo
hauna tofauti na mikataba yoyote ya
Liverpool na kuwa makubaliano yatafikiwa
kabla ya Jumanne (Express),
Arsenal
wanafikiria kumchukua Toby Alderweireld,
25, kutoka Atlètico Madrid kuziba nafasi ya
Thomas Vermaelen aliyekwenda Barcelona
(Star),
Gunners pia wanamfuatilia beki wa
Olympiakos Kostas Manolas, 23, ambaye
alichezea Ugiriki katika Kombe la Dunia na
ambaye anatazamwa pia na Man U (Express),
kipa wa Chelsea Petr Cech, 33, anajiandaa
kuondoka Darajani baada ya nafasi yake
kuchukuliwa na Thibault Courtois (Mail on
Sunday),
Lukas Podolski anajiandaa kuondoka
Arsenal na kwenda Juventus kwa mkopo
(Sunday Express),
Arsene Wenger alimkataa
mara mbili Mario Balotelli anayekwenda
Liverpool. Balotelli angeweza kwenda
Emirates kama Wenger angemtaka (Metro),
Valencia wanataka kumsajili Alvaro Negredo
kutoka Manchester City kabla ya dirisha la
usajili halijafungwa, pia wanawafuatilia
Fernando Llorente na Anthony Martial
(Superdeporte).
Zimesalia siku nane kabla ya
dirisha la usajili kufungwa.
0 comments:
Post a Comment