Nchini
Kenya kuna Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Naivasha ambae katengeneza
‘Ndege’ yake ambayo toka ameanza kuiunda alisema lazima ipae huku akiwa
katumia vifaa mbalimbali kutoka kwenye Bajaji kuiunda.
Mzigo ulipokamilika nyumbani kwao alipoitengenezea, Polisi wa mji huo
wakamkataza kuipaisha kwa sababu ni kinyume na sheria lakini ili kuepuka
kumkatisha tamaa… wakamwambia ni vyema akapata kibali kutoka kwa
mamlaka ya anga.
Paul Karanja alizuiwa na polisi kuipaisha hii ndege kutoka uwanja wa
mdogo wa ndege wa Karagita na kuwanyima uhondo zaidi ya watu 500
waliofika asubuhi ya saa 3 kuangalia chombo kikipaishwa.
Hata
hivyo Mwanachuo huyu wa chuo kikuu cha Meru ana imani ataipaisha ndege
yake siku moja ili kutimiza ndoto yake ambayo hata hivyo ilipata
hitilafu kwenye uwanja wa ndege wa Karagita kutokana na hali mbaya ya
uwanja huu iliyosababisha tairi la ndege yake kuharibika.
Karanja ambae ni Mwalimu pia wa shule ya upili, amesema tayari
ameiandikia barua mamlaka ya ndege nchini Kenya kuhusu kupaisha ndege
hiyo lakini hajapata majibu.
0 comments:
Post a Comment